Nenda kwa yaliyomo

Majadiliano:Çanakkale

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Afya, Utalii na Uturuki

[hariri chanzo]

Mwezi wa Januari 2016, mtumiaji fulani alitafsiri insha mbalimbali kutoka redio ya Kituruki. Makala zake zimefutwa sasa, lakini habari zifuatazo zinagusa mada ya mji wa Canakkale. Labda ingefaa kuyaingiza baadhi ya maneno au habari katika makala hii ya mji huo. --Baba Tabita (majadiliano) 12:49, 20 Oktoba 2016 (UTC)[jibu]

Mji wa Canakkale
Historia ya Mji wa Çanakkale ambao unaziunganisha bahari mbili, bahari ya Ege na bahari ya Marmara inaelezewa kuwepo tangu kale. Kama lilivyo jiji l Istanbul, Çanakkale pia inapatikana katiika pande za bara la Ulaya na bara la Asia. Kwa miaka Zaidi ya elfu, mji huu umeongozwa na dola mbalimbali, na hivyo kubeba ustaarabu wa aina mbalimbali.
Tunapouzungumzia mji wa Çanakkale na historia yake bila shaka akilini mwetu unatujia mji wa kale, mji wa Troy. Ukiwa katika mlima Hirsarlık katika upande wa Asia wa mji wa Çanakkkale, mji huu unasemekana kuwa uliasisiwa mnamo miaka 3000 kabla ya Kristu.
Uchunguzi wa kiakolojia ambao ulifanywa katika karne ya 19 umeonyesha kuwa kulikua na matabaka 9 ya miji katika udongo huo. Kutokakana na kukaliwa na watu wa ustaarabu mbalimbali, pamoja na nafasi yake kijografia, Troy imekua katika orodha ya urithi wa dunia ya UNESCO tangu mwaka 1998.
Akiwa ni mmoja wa washairi wakubwa wa Kigiriki, Homa ndiye mtu aliyeupa umaarufu mkubwa mji wa Troy duniani. Kwakua Homer alinukuliwa katika kazi yake ya Iliad akisema kuwa chanzo kikuu cha kazi za fasihi za Magharibi ni vita maarufu ya troy ambayo ilitokea mjini Troy.
Baada ya kuona kuwa wanashindwa vita hivyo, Wagiriki wakatengeneza sanamu kubwa ya farasi wa mbao na wakaficha ndani yake kundi kubwa la askari. Watu wa Troy wakalichukua sanamu hilo kwa furaha na kulipeleka mpaka katikati ya mji kama alama ya ushindi. Askari waliomo ndani ya sanamu hilo walitoka nyakati za usiku na kuwafungulia askari wengine wa Kigiriki mageti ya mji wa Troy. Mji wa Troy ukaangukia mikononi mwa Ugiriki usiku huo na Ugiriki ikashinda vita.
Mji wa Troy umekua gumzo kubwa duniani hasa katika kipindi cha miaka 10 iliyopita hususan kufuatia kutengenezwa kwa filamu ya “The Troy” ya mwaka 2004 huku muigizaji wake mkuu akiwa ni Brad Pitt.
Uchunguzi unaendelea mpaka hivi sasa katika mji huu wa kale wa Troy, ambao unatembelewa na maelfu ya watalii kila mwaka. Kila matokeo ya utafiti yakitoka yanaleta mwanga mwingine wa elimu kuhusiana na mji huo na kutupa wasaa Zaidi wa kuujua mji huo.
Çanakkale ambayo inautajiri mkubwa wa historia na mi ambao unajumuisha miji mingine 30 ya kale, pia imejaaliwa kwa vyanzo vya nishati ya mvuke. Kuna chemchem nyingi za maji ya moto katika mji huu. Moja ya chemchem hizo ambayo ni maarufu na imetumika kwa miaka Zaidi ya elfu, ni ile chemchem ya Kestanbol inayopatikana katika wilaya ya Erzine.
Ikiwa takriban kilomita 65 kutoka katika kitovu cha mji wa Çanakkale, Kestanbol inahesabika kuwa ni moja ya chemchem kongwe kabisa nchini Uturuki. Chemchem ya Kestanbol ambayo inapatikana katika mipaka ya mji wa zamani wa Alexandria Troas, inaaminika kuwa ikitumika kwa Zaidi ya miaka 2300 sasa.
Mji wa Alexandria Troas ni mji mkongwe ambao ulianzishwa mnamo mwaka 310 Kabla ya Kristo ili kumsifu Alexander the Great. Zamani chemchem za Kestanbol zilitumika kuwatibu watu wa mji huo.
Mji huo ulipotekwa na dola ya Warumi, zilitengenezwa sehemu za kuogea karibu na chemchem hizo. Mji huu unabaki kuwa na umuhimu mkubwa hata katika hisoria ya dola ya Ottoman. Hadithi zisizo za kusadikika zinasema kuwa mfalme Suleyman the Magnificent alikua akiwatibu majeruhi wa vita kwa kutumia maji ya chemchem hii. Ya Kestanbol.
Wakazi wa mji huu wa Alexandria Troas wameyapa maji hayo jina la maji yanayofufua wafu. Imani hii inahusishwa na historia za kidini. Inasimuliwa kuwa mnamo mwaka 52 kabla ya Kristo, swahaba mmoja wa Yesu, Mtakatifu Paulo aliamua kusafiri kutoka Anatolia kuelekea Ulaya. Akafika katika bandari ya mji huu wa Alexandria Troas na kuanza kuhubiri. Mvulana mmoja ambaye alikua akimsikiliza kupitia dirisha la nyumba yake alidondoka na kufariki. Akachukuliwa hapohapo na kupelekwa katika maji ya Kestanbol na baadaye alirudi kuwa hai.
Unaendelea kusikiliza kipindi chako cha afya, utalii na Uturuki kinachokujia kupitia idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Uturuki. Leo hii tumezungumzia chemchem ya Kestanbul inayopatikana katika wilaya ya Ezine mjini Çanakkale.
Chemchem ya Kestanbol ambayo inapakana na bahari kwa bustani ya mizeituni na miti mblimbali, inaendelea kutibu watu kama ilivyotibu miaka Zaidi ya elfu moja iliyopita. Joto la maji ya Kestanbol ambayo yana madini mengi ya chumvi, Klorini, madini ya chuma, floridi na madini yenye mionzi ni kati ya nyuzijoto 54 na 75. Chanzo hiki kuitwa ni “maji ya chuma” kutokana na kuwa na kiwango kikubwa cha madini. Aidha pia huitwa “maajabu ya ujana kutokana na kuwa na kiwango kidogo cha mionzi.
Utafiti wa maji hayo ambayo yanatoka katika vyanzo sita tofauti unaonesha kuwa maji hayo yana uwezo mkubwa wa kutibu magonjwa mbalimbali kama vile magonjwa ya ngozi, matatizo ya uzazi, matatizo ya tumbo, matatizo ya misuli, na mfumo wa fahamu na matatizo ya kibofu cha mkojo.
Ukiachana na tiba, chemchem hii ya Kestanbol ipo sehemu ambayo ni nzuri kw watu kupumzika kimwili na kiakili kwakua inawapa nafasi watalii kuona mambo ya kihistoria na kiasili.
http://www.trt.net.tr/swahili/uturuki/2016/01/01/afya-utalii-na-uturuki-447170