Wikipedia:Makala kwa ufutaji/Nyaraka 1
Hii ni nyaraka za makala Wikipedia:Makala kwa ufutaji kwa miaka ya 2006 hadi 2010.
Mradi wa Kamusi ya Kimarathi na Kiswahili
[hariri chanzo]Je tufanye nini na makala ya kamusi hiyo??? Nilivyoandika kwenye ukurasa wa majadiliano ya kamusi:
Sijaelewa sababu ya makala hii: Haielezi kamusi lakini inavyoonekana inajaribu kuanzisha kamusi hiyo. Je, iwe sehemu ya kamusielezo ya Kiswahili? Au mahali pake ni penye mradi mwingine? Sisemi ifutwe kabisa bali isogezwe kwenye mradi mwingine wa wikipedia. --Oliver Stegen 17:11, 19 Machi 2007 (UTC)
Hakuna yaliyomo ingawa kuna makala ya Kiingereza (angalia [1]). Kama hakuna atakayetafsiri makala kutoka Kiingereza, itafutwa. --Oliver Stegen 13:08, 17 Aprili 2007 (UTC)
- Imefutwa (nadhani nimesubiri muda wa kutosha). --Oliver Stegen 10:03, 22 May 2007 (UTC)
Makala hii haina maneno, tena maelezo yake ya kwanza (angalia historia ya makala) kwamba ni kifupisho cha "Zimbabwe Industrial Index" sijaweza kuyahakikisha. Kwa vyovyote, hakuna makala ya "index" hiyo. Kama hakuna atakayetoa sababu ya kutokufuta makala hii, nitaifuta baada ya siku kadhaa. --Oliver Stegen 10:35, 22 Machi 2007 (UTC)
- Haya, imefutwa. --Oliver Stegen 14:06, 31 Machi 2007 (UTC)
Lugha ya kwanza
[hariri chanzo]Makala hii haielezi kitu kuhusu lugha bali ni uharabu tu. Ifutwe. --Oliver Stegen 14:41, 7 Februari 2007 (UTC)
- Haya, nimeshaandika maelezo yanayoleta maana - maana yake, isifutwe! --Oliver Stegen 17:18, 19 Machi 2007 (UTC)
Nimegundua tena makala nyingine ambayo nimeshauri ifutwe (kwenye ukurasa wa majadiliano ya Ndesanjo) wiki kadhaa zilizopita:
- Naomba ufute makala hii: Insert text. Haieleweki inarejea nini, na jina lake ni Kiingereza. Asante, --Oliver Stegen 08:53, 22 Januari 2007 (UTC)
Jamani, kuna mwenye kuelewa maana ya makala hii? Nimeisoma nikashindwa kuielewa: http://sw.wikipedia.org/wiki/Semsem_Barabara -- --Ndesanjo
- Inavyoonekana hii ni tafsiri ya mashine ya makala katika wikipedia ya Kiingereza kuhusu maonyesho ya televisheni yaliyoanzishwa Marekani, yaani "Sesame Street", au kwenye Afrika ya Kusini ni "Takalani Sesame" [[2]]. Kama hakuna atakayesikia umuhimu wa kuitafsiri sawasawa, na ifutwe. --Oliver Stegen 23:22, 1 Februari 2007 (UTC)
- Nimeifuta. Matt Crypto 20:34, 4 Februari 2007 (UTC)
Nimegundua tena ukurasa mwingine ambao ufutwe:
- Hakuna Kiswahili katika kiungo hiki, ukurasa huu ufutwe. --Oliver Stegen 20:23, 17 Agosti 2006 (UTC)
- Nimeifuta. Matt Crypto 20:34, 4 Februari 2007 (UTC)
Na mwingine tena:
- Huyu Evan Carroll ni nani? Siwezi kumkuta kwenye wikipedia nyingine. Kama hajulikani au hana umuhimu, makala hii ifutwe tena. Poleni! --Oliver Stegen 22:52, 3 Oktoba 2006 (UTC)
- Nimeifuta. Matt Crypto 20:34, 4 Februari 2007 (UTC)
Mimi ningependekeza kufuta makala Benzi karl fredrick kwa sababu mbili: A) mtu huyu alikuwa na jina kamili ndilo "Carl Friedrich Benz". Tusianze aina hii ya lugha tafadhali - baadaye tutapata "Bushi Georgi" au "Churichilli Winisitoni" au hata "Muwarimu Niyelele" kwa sababu mtu fulani anataka kuingiza lahaja ya nyumbani au tatizo lake la kutamka herufi fulani akidai kasoro yake ndicho Kiswahili chenyewe!! B)makala inajaa makosa - Benz haikuwa mtu wa kwanza aliyetengeneza injini ya petroli. Kwa sababu ya jina la makala ni la makosa haina faida kusahihisha makosa yaliyomo --Kipala 23:35, 26 Januari 2006 (UTC)
- Imehamishwa. Matt Crypto 23:53, 31 Januari 2007 (UTC)
ifutwe!! --Kipala 17:41, 6 Februari 2006 (UTC)
Hii si makala ya Kiswahili, ila maneno machache yameyotafsiriwa. Matt Crypto 13:54, 21 Aprili 2006 (UTC)
- Sasa ni makala ya Kiingereza tu. Napendekeza ifutwe. Matt Crypto 07:00, 26 Aprili 2006 (UTC)
- Haya, Kipala ameitafsiri. Matt Crypto 18:55, 26 Aprili 2006 (UTC)
Nilivyoandika miezi kadhaa iliyopita:
- Huyu Bobbie Thompson ni nani? Siwezi kumkuta kwenye wikipedia nyingine. Kama hajulikani au hana umuhimu, makala hii ifutwe tena. Poleni! --Oliver Stegen 22:53, 3 Oktoba 2006 (UTC)
Ifutwe kwa vile siyo Kiswahili. --Oliver Stegen 12:33, 22 Januari 2007 (UTC)
Ifutwe kwa vile ina maneno matatu tu. Pia, kichwa chake hakina maana (taira iwe taifa labda?). Ikiwa makala hii inarejea nembo ya Tanzania, ifuate mfano wa Nembo ya Mexiko. --Oliver Stegen 11:28, 31 Januari 2007 (UTC)
Mwongozo - IBAKI!
[hariri chanzo]Makala hii ni sentensi ya kwanza ya makala kuhusu Peter Tosh tu. Haielezi chochote kuhusu "mwongozo". Ifutwe. --Oliver Stegen 12:06, 31 Januari 2007 (UTC)
- Siku hizi ni sawa, yaani ni kuhusu kata mkoani Tabora. Asante! --Baba Tabita (majadiliano) 14:35, 26 Agosti 2009 (UTC)
Ni uharabu tu. Ifutwe. Tena, tunahitaji msaada wa kuzuia au kurekebisha uharabu. --Oliver Stegen 15:33, 31 Januari 2007 (UTC)
Ni picha tu, na kiungo cha makala ya wikipedia ya Kireno. Haileti maana. Ifutwe. --Oliver Stegen 15:44, 31 Januari 2007 (UTC)
Makala inaeleza jambo muhimu lakini hailingani kabisa na masharti ya Kamusi elezo.
- Haina mpangilio wa kamusi lakini imefanana na makala ya gazeti au zaida hotuba
- Lugha haifai katika kamusi, mfano: "Nimesema tayari alituzwa na Zawadi ya Nobel..." ; "Si rahisi kupata tuzo nyingi kama hizi; kweli yeye ni shujaa."
- Mpangilio haisaidii wasomaji wapate haraka habari za kimsingi
Ilhali mada ni muhimu: Nani atahariri ? --Kipala 05:47, 27 Aprili 2007 (UTC)
- Nimehariri makala. --Oliver Stegen 14:13, 27 Aprili 2007 (UTC)
- Safi !! --Kipala 09:11, 28 Aprili 2007 (UTC)
Dismas Lyassa, ni Mtanzania, mwandishi wa habari, aliyezaliwa Juni 26, 1976, katika kijiji cha Mofu, Ifakara, mkoani Morogoro-Tanzania. Nchini Tanzania, Dismas Lyassa anaheshimika hasa kutokana na uwezo wake mkubwa katika kutoa ushauri kwa jamii kwa njia ya magazeti na vyombo vingine vya habari. Pia anasifika kwa kuanzisha vituo kadhaa vya ushauri nchini Tanzania, kupitia taasisi yake aliyoianzisha ya Global Source Watch, aliyoainzisha toka mwaka 2001. Nje ya kuwa mwanzilishi wa mashirika kadhaa yasiyo ya Kiserikali na makundi ya kidini akitumia majina ya watu wengine, kwa lengo la kusaidia ustawi wa Tanzania, Dismas Lyassa, kwa ujumla anaonekana ni mtu mwenye uwezo mkubwa katika kutoa ushauri, kiasi kwamba mwaka 2012 februari, alichaguliwa kwenda Marekani katika mpango maalum wa kuwafundisha waandishi wa habari ili waweze kuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kuwasaidia Watanzania kupitia maandishi. Kazi zake zimesababisha ashinde tuzo kadhaa zikiwemo Mwandishi bora katika habari za uchunguzi mwaka 2007 Tanzania nzima. Watanzania wengi wanamuona Dismas Lyassa, kama ni mtu mwenye uwezo mkubwa katika kusaidia jamii na kwamba akipewa nafasi kubwa zaidi anaweza kuleta mabadiliko makubwa kwa jamii ya Tanzania, kwani kupitia makala zake amekuwa akishauri vizuri mno na kuna wengi wamebadili staili za maisha yao kupitia makala zake. Akiwa baba mwenye watoto wawili, Dismas hupenda kutia moyo watu, na hilo limekuwa ni jambo lenye kufurahisha wengi. Katika maisha kwa hakika ni kioo, kwa sababu hata kufanikiwa kwake haikuwa rahisi, kwani ni mtu aliyetokea familia duni mno, kiasi kwamba katika mojawapo ya machapisho yake alikiri kwamba kuna wakati akiwa kijijini kwao, mvua iloilipokuwa inanyesha, ilikuwa inasababisha ajute, kwa vile nyumba ambayo alikuwa analala, ilikuwa inavuja.
Uteuzi wa Kufutwa kwa Makala ya Listen
[hariri chanzo]Jamani Naomba ifutwe mara moja maana hakieleweki nini mieandikwa. Kwanza makala haijafuata kanuni na taratibu za kamusi elezo inavyosema hivyo haina haki ya kuwa katika moja kati ya makala za Wikipedia naomba ifutwe. Ahsanteni.--Muddyb Blast Producer 12:05, 15 Oktoba 2007 (UTC)
Makala hii kuna habari za binafsi zinazofaa kwa ukurasa wa mtumiaji lakini si kwa makala. Mtumiaji ameelezwa tatizo. --Kipala 22:47, 29 Oktoba 2007 (UTC)
iwe ukurasa wa mtumiaji (user-page)
Ifutwe. Haieleweki. Ndesanjo 18:22, 10 Novemba 2007 (UTC)
Samahanini Nd. Wakabidhi. Makala hii niliingiza kwa bahati mbaya, sikuwa na maana ya kutaka kuiweka. Lengo langu lilikuwa kutaka kuumba Jamii "Waigizaji wa Filamu Marekani" na sio kuweka katika makala, hivyo napendekeza ifutwe tu. Natanguliza kusamehewa kwangu kwenu. Ni mimi mchangiaji wenu.--Mwanaharakati 13:01, 17 Novemba 2007 (UTC)
Makala haina maana haielezi kichwa chake halafu inatangaza ama kampuni au ofisi ya binafsi; hailingai na masharti ya kamusi --Kipala 14:56, 24 Novemba 2007 (UTC)
Hii ilikuwa makala ya kujaribia template:filamu wakati wa uundaji wa template hiyo, hivyo yaweza kufutwa maana haina kazi tena.--Mwanaharakati 16:19, 26 Novemba 2007 (UTC)
Hamna cha maana kilicho wekwa wala lolote lile lenye kufanya makala hii kuwepo. Kwanza nani atakaekuja hapa kutafuta hao Wamarekani? Pili hatuna utaratibu wa kuweka dot com katika makala zetu hivyo ifutwe mara moja. --Mwanaharakati 16:36, 10 Desemba 2007 (UTC)
Kuna mwenye kufahamu lolote kuhusu hii:WP:AIV, na kama hakuna wa kuielezea kwa kirefu, basi ifutwe!! Maana hakuna kilichoandikwa!!--Mwanaharakati 14:03, 21 Januari 2008 (UTC)
Hamna cha maana hasa kilichoandikwa katika ukurasa huo, zaidi ya matusi na kejeri juu ya wiki hii. Ningeshauri ifutwe.--Mwanaharakati 12:30, 24 Januari 2008 (UTC)
Wakti umepita wa kusubiria marekebisho ya makala hiyo. Kama kuna mmoja wetu anaweza kuuelezea muziki wa Burundi, basi auelezee!! Endapo itakuwa hamna yoyote yule anayejua habari kuhusu muziki wa Burundi, basi napendekeza makala ifutwe!!!!--Mwanaharakati (talk) 14:43, 19 Februari 2008 (UTC)
Msaada:Yaliyomo - IBAKI!
[hariri chanzo]Na hii ndiyo nini? Naona hamna cha maana kilichoandikwa. Naomba makala hiyo ipelekwe Pugu Machinjioni ikachinjwe. Napendekeza ifutwe..--Mwanaharakati (talk) 14:46, 19 Februari 2008 (UTC)
- Imerekebishwa kuelekea faili ya msaada husika. --Baba Tabita (majadiliano) 14:37, 26 Agosti 2009 (UTC)
Kichwa cha habari hapo juu, ni habari inayomhusu mwanamama mmoja aliyeweka habari zake katika sehemu isiyotakiwa. Natumai atakuwa hajui lolote kuhusiana na Wikipedia, lakini nimeshamtumia e-mail ili aweze kuhondosha yale maelezo yake katika ukurasa huo na azipeleke katika ukarasa wa binafsi! Pia ajiunge na wikipedia ili aweze kuweka habari zile katika username space. Nasubiria majibu ya e-mail yake ili ukurasa uweze kuhondoshwa katika sehemu ile. Sina la zaidi..--Mwanaharakati (majadiliano) 09:53, 31 Machi 2008 (UTC)
Bongo Records - INABAKI!
[hariri chanzo]Haina Kiswahili ndani yake sijui kama Kiarabu kile kina maana au la - ikae siku tatu. --Kipala (majadiliano) 10:45, 6 Julai 2008 (UTC)
- Imetafsiriwa na Muddyb yaani isifutwe sasa. Asante! --Baba Tabita (majadiliano) 18:36, 27 Julai 2008 (UTC)
- (sw) Ni kweli. Nimeiandikia makala, ingawaje habari zake si ndefu sana. Niko najaribu kuwasiliana nao ili niweze kupata habari zao zaidi!! Si inaswihi? --Mwanaharakati (majadiliano) 14:46, 18 Agosti 2008 (UTC)
Nimejaribu kutafuta habari zaidi kuhusu mtu huyu ila siwezi kumpata mtandaoni popote. Kama hakuna habari nyingine ambayo ingethibitishwa rasmi (pamoja na wasifu yake au orodha ya albamu zake), makala hii ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 17:58, 28 Agosti 2008 (UTC)
- Huyo kweli maarufu hakuna mfano, lakini kama unavyojua watu wa Tanzania mambo ya mtandao wao wapo "zero". Tazama hii:
Utaona filamu aliongoza na kutunga mwenyewe. Jamaa anatamba sana nchini, lakini kama nilivyosema kuwa watu wa Bongo kuhusu mtandao, wao empty. Basi hata ile ya bure, pia hawajushughulishi nayo! Hivi karibuni katoa filamu kadhaa:
- Engagement Day
- Penina
- Why Me
Na nyingine nyingi alizofanya bwana huyu!--Mwanaharakati (majadiliano) 06:33, 29 Agosti 2008 (UTC)
- Kama huyo ni maarufu hivyo naomba utupanulie habari zake katika makala; nami nitatoa ombi la kufuta ;-) Wasalaam, Baba Tabita (majadiliano) 19:00, 31 Agosti 2008 (UTC)
Eti, anasema kama unataka kutoa hoja zako kuhusiana ufisadi Tanzania. Kwani hapa ndiyo pakufanyia majadiliano ya ufisadi wa hao viongozi wa Tanzania? Chakushangaza, huyu bwana yeye ni mwandishi wa Habari wa Gazeti fulani hivi ambalo kwa jina nimelisahau, lakini ni mwandishi wa Habari. Nitamweleza kujiandika vyema na sio kuandika zile habari zisizohusiana na kamusi elezo!--Mwanaharakati (majadiliano) 10:17, 8 Septemba 2008 (UTC)
Eti Mbuni Somali ndiyo nini? Miye sijui hata kidogo. Labda wakubwa wakazi mnajua hii ni kitu gani, hivyo nilikuwa naomba nifahamishwe! Ikionekana hakijulikani ni kitu gani, basi ifutwe!!--Mwanaharakati (majadiliano) 14:21, 10 Septemba 2008 (UTC)
Hafsa Kazinja - IBAKI!
[hariri chanzo]Makala ya mtu huyo haina habari ambazo zingestahili ziwemo katika kamusi elezo. Tena, sentensi yake moja iliandikwa zaidi ya mwaka mmoja uliopita. Kama hakuna atakayeweza kuongeza habari, makala hiyo itafutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 14:05, 15 Septemba 2008 (UTC)
- Jamii, marejeo na picha zimeongezwa. Nashukuru! --Baba Tabita (majadiliano) 14:37, 23 Januari 2009 (UTC)
Makala nyingine ambayo haina habari zifaazo kwa kamusi elezo. Nayo itafutwa isipoongezewa. --Baba Tabita (majadiliano) 15:09, 18 Septemba 2008 (UTC)
- Sijui lolote kuhusu huyo! Ifutwe tu.--Mwanaharakati (Longa) 11:59, 29 Septemba 2008 (UTC)
Sijafuta moja kwa moja kwa sababu haina nia mbaya ila tu mwandishi hana habari jinsi ya kutunga makala ya wikipedia. Makala inaweza kubaki akiongeza:
- a) mwaka wa kuzaliwa; anakotoka, elimu...
- b)mhusika ni msanii wa aina gani, amefanya nini;
- c)anafanya kazi tangu lini na wapi na vingine kadhaa.
Kama hayaongezwi itafutwa. --Kipala (majadiliano) 20:19, 28 Novemba 2008 (UTC)
- Kwa vile hakuna aliyeweza kuongeza kitu karibu kwa miezi miwili, sasa imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 14:40, 23 Januari 2009 (UTC)
Inaonekana imenakiliwa kutoka kitabu lakini wapi? Kama hakuna anayejua faida ya makala iende.--Kipala (majadiliano) 10:59, 30 Novemba 2008 (UTC)
Hakuna kitabu cha namna hiyo. Aliyeandika makala hii ni mimi mwenyewe. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 08:04, 12 Aprili 2009 (UTC)
Rama mpili
[hariri chanzo]Huyu bwana simjui wala sijawahi kumsikia habari zake. Nadhani kaamua kujitangaza, lakini mfumo aliotumia si mzuri! Alitakiwa ataje mwaka wa kuzaliwa na historia ya maisha katika kazi zake. Napendekeza ifutwe!--Mwanaharakati (Longa) 12:54, 29 Desemba 2008 (UTC)
- Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 08:13, 7 Februari 2009 (UTC)
- ISIFUTWE - Huyu bwana mimi namjua ni mtanzania sasa anaishi ughaibuni nchini Australia ni msanaii mzurii wa sculpture pia ni mwalimu wa art uko Australi nilikuwa nae chuo Amstadam,nashauri msifute ili nijalibu kuwasiliana nae ikiwa kama kaandika yeye au mtu mwengine (kati ya wanafunzi wake)hatuwekee kila kitu na intress kwa wasomaji natuma mtafurahi kwa ninavyo njua. --85.24.200.24 15:06, 11 Agosti 2009 (UTC)
- Sawa, ukiweza kupata habari au kuandika wasifu ya huyo msanii, uanzishe upya kwa kubonyeza kiungo cha Rama Mpili hapa. Makala ya zamani ilifutwa tayari miezi kadhaa iliyopita. Pole! --Baba Tabita (majadiliano) 22:04, 11 Agosti 2009 (UTC)
Salaam, Wanawikipedia. Mtanisamehe kwa kuziweka kitangazo cha ufutaji juu ya makala hizi mbili. Masuala ya kutaka kuandika makala za filamu yanahitaji mambo mengi mno kiasi kwamba si rahisi kwa filamu za Tanzania kuweza kuandikwa katika Wikipedia - ilhali wao wenyewe hawataki kudhihirisha hali halisi ya washiriki ama wajenzi wa filamu. Mambo hay ni pamoja na kuweka kitu kama:
- Washiriki
- Wahariri
- Waongozaji/mwongozaji
- Wasambazaji
- Watayarishaji
Na mengine mengi tu yanatakiwa yawepo kwenye filamu. Makala haijataja filamu imetolewa mwaka ama kutengenezwa. Makala haijataja nani mwigizaji kiongozi wa filamu hii. Hivyo ninapendekeza makala zote zifutwe, maanake hatuwezi kuandika vitu ambavyo haviendani na mwenendo wa kamusi elezo ya Wiki vile inavyosema. Wenu mtiifu,--Mwanaharakati (Longa) 05:54, 16 Februari 2009 (UTC)
- Nakubali jinsi ilivyo haifai kabisa. Kama hakuna anayeweza kuibadilisha kuwa makala halali basi ifutwe hata nikiona hasara ya kufuta makala juu ya filamu ya Kitanzania. Lakini si vema kama makala juu ya filamu ya Kitanzania ni bovu na zile juu ya filamu za nje ni safi. Heri iende. Tusubiri wiki moja. --Kipala (majadiliano) 13:53, 16 Februari 2009 (UTC)
Maelezo yake sawa tu na hayo ya juu! Mwandishi ni yuleyule. Ziende tu, kwani mwandishi mbishi - na wala hataki kuomba msaada kwa watu walionauzoefu walau waweze kutoa michango yao juu ya matumizi au uandishi wa makala za Wikipedia hasa kwenye masuala ya filamu.--Mwanaharakati (Longa) 15:03, 16 Februari 2009 (UTC)
Kuna mwenye kujua lolote kuhusiana na hii? Kama hakuna, basi ifutwe!--Mwanaharakati (Longa) 11:29, 27 Machi 2009 (UTC)
- Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 14:17, 18 Mei 2009 (UTC)
Ni neno la Kizulu, tena ni sentensi moja tu. Haina kiungo pengine wala haiungwi kutoka ukurasa mwingine. Isipopanuliwa hivi karibuni, na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 10:20, 22 Mei 2009 (UTC)
- Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 21:26, 9 Julai 2009 (UTC)
Makala hii haiandikwi kwa Kiswahili bali kwa Kiswidi tu. Haina kiungo pengine wala haiungwi kutoka ukurasa mwingine. Isipotafsiriwa hivi karibuni, na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 10:20, 22 Mei 2009 (UTC)
- Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 21:26, 9 Julai 2009 (UTC)
Ni mda sasa nilikuwa nikisubria makala hii kufanyiwa marekebisho, lakini hadi sasa hamna chochote kile kilichowekwa sawa. Naomba ifutwe maana hamna kilichoandikwa cha msingi sana, ambacho kitapelekea makala hii kuwepo. Ahsante.--Mwanaharakati 11:28, 12 Novemba 2007 (UTC)
Sina ufahamu na kilichoelewa humo. Kama kuna mwenye kuelewa, basi asawazishe - vingenevyo ifutwe!!--Mwanaharakati (Longa) 16:40, 22 Mei 2009 (UTC)
- Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 21:26, 9 Julai 2009 (UTC)
Makala hii ina maneno matatu tu. Haifai kwa kamusi elezi. Tena, "manjano" kwa Kiswahili siyo rangi hasa bali ni kiungo chenye rangi ya manjano. Makala isipopanuliwa lazima ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 21:23, 9 Julai 2009 (UTC)
- Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 22:14, 11 Agosti 2009 (UTC)
Penitenciaría Federal de Sona - IBAKI!
[hariri chanzo]Makala hii haijaleta maana. Ni tafsiri ya sentensi tatu tu kutoka wikipedia nyingine kuhusu jela katika filamu fulani. Isipopanuliwa ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 13:00, 22 Agosti 2009 (UTC)
- Hii ninaishughulikia kwa sababu ninaijua namna ya kuielezea. Zingine nimejaribu kuzitazama nimeona mauzauza tu, basi zifutwe. Hazina mwelekeo wa kikamusi elezo.-- MwanaharakatiLonga 13:16, 25 Agosti 2009 (UTC)
Bila habari kuhusu muungano huo, makala haifai kwa kamusi elezo na ifutwe. Naomba mtu aiongezee. --Baba Tabita (majadiliano) 14:21, 24 Agosti 2009 (UTC)
- Imefutwa! --Baba Tabita (majadiliano) 10:35, 11 Oktoba 2009 (UTC)
Kuna mwenye kujua lolote kuhusiana na makala tajwa hapo juu? Binafsi sielewi - ninapendekeza ifutwe.-- MwanaharakatiLonga 05:10, 29 Agosti 2009 (UTC)
- Ifutwe tu. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 18:35, 29 Agosti 2009 (UTC)
- Imefutwa. Sj (majadiliano) 08:10, 18 Septemba 2009 (UTC)
Makala hii bado sana, ni sentensi moja tu bila habari zifaazo kwa kamusi elezo. Bila habari nyingine zitakazowekwa katika taratibu, na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 14:26, 24 Agosti 2009 (UTC)
- Imefutwa. Sj (majadiliano) 08:08, 18 Septemba 2009 (UTC)
Siyo makala bali barua yenye maswali ya kibinafsi. Tena, habari zote zimo kwenye makala ya Yesu. Kama hakuna atakayekataa itafutwa baada ya muda. --Baba Tabita (majadiliano) 14:52, 24 Agosti 2009 (UTC)
- Ifutwe tu. --196.45.46.171 12:08, 25 Agosti 2009 (UTC)
- Imefutwa. Sj (majadiliano) 08:10, 18 Septemba 2009 (UTC)
Kichwa cha makala hiyo siyo Kiswahili sanifu, na hata mwandikaji mwenyewe amesema ifutwe kama utafsiri wake umekoseka. Imefutwa! --Baba Tabita (majadiliano) 10:35, 11 Oktoba 2009 (UTC)
Ifutwe a) lugha si Kiswahili b) si makala ya kamusi c) imenakiliwa mahali --Kipala (majadiliano) 19:34, 27 Novemba 2009 (UTC)--91.98.113.164 19:33, 27 Novemba 2009 (UTC)
Ukurasa mkami. Jon Harald Søby (majadiliano) 12:12, 2 Desemba 2009 (UTC)
Makala hii haijaanzishwa bado. Ina kiungo kwa ukurasa wa kuuhariri tu. Kama hakuna ambaye angeweza kuingiza habari kuhusu Oliech (je, ni nini au nani?), na ifutwe! --Baba Tabita (majadiliano) 16:45, 3 Januari 2010 (UTC)
- Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 14:04, 29 Januari 2010 (UTC)
Makala nyingine bila yaliyomo tangu kuanzishwa tarehe 21 Novemba 2009. Ifutwe! --Baba Tabita (majadiliano) 14:03, 29 Januari 2010 (UTC)
- Nakubali. Imeenda. --Kipala (majadiliano) 15:53, 9 Februari 2010 (UTC)
Na nyingine vilevile. Ifutwe! --Baba Tabita (majadiliano) 14:03, 29 Januari 2010 (UTC)
- Nakubali. Imeenda. --Kipala (majadiliano) 15:53, 9 Februari 2010 (UTC)
Nyingine tena. Ifutwe! --Baba Tabita (majadiliano) 14:03, 29 Januari 2010 (UTC)
Makala hii haina yaliyomo tangu ilianzishwa tarehe 25 Novemba 2009. Tena, jina la familia liandikwe na herufi kubwa. Kama hakuna ambaye angeweza kuongeza habari ya mtu huyo, makala ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 18:20, 1 Februari 2010 (UTC)
- Nimegundua jina hilo ni jina la mshiriki wa KWC. Naona haikuwa nia yake kujianzishia makala katika kamusi elezo, na makala imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 12:04, 2 Februari 2010 (UTC)
Jamii nkami, iliipokea Jamii:Kijisehemu nchi kwa nchi. Jon Harald Søby (majadiliano) 11:43, 12 Novemba 2009 (UTC)
- Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 06:04, 10 Februari 2010 (UTC)
Haina yaliyomo tangu ilipoanzishwa tarehe 24 Novemba 2009. Tena, sina uhakika kama makala yenye kichwa hiki ni lazima. Machoni mwangu ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 05:26, 29 Januari 2010 (UTC)
- Nakubali. Imeenda --Kipala (majadiliano) 11:13, 10 Februari 2010 (UTC)
Haina yaliyomo tangu ilipoanzishwa tarehe 21 Novemba 2009. Labda mtu aweza kutafsiri kutoka en:Corruption. La sivyo, na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 05:29, 29 Januari 2010 (UTC)
- Nakubali. Imeenda. --Kipala (majadiliano) 15:53, 9 Februari 2010 (UTC)
- Mbona bado ipo? Umebadilisha mawazo na kupanga kuitafsiri kutoka Kiingereza? --Baba Tabita (majadiliano) 05:59, 10 Februari 2010 (UTC)
- Nakubali. Imeenda SASA --Kipala (majadiliano) 11:13, 10 Februari 2010 (UTC)
Ingefaa kujaza makala hiyo lakini tangu uanzishaji wake tarehe 21 Novemba 2009 hakuna. Isipopanuliwa, na ifutwe --Baba Tabita (majadiliano) 03:46, 30 Januari 2010 (UTC)
- Haya, mkuu! Imetekelezwa. --Kipala (majadiliano) 17:12, 9 Februari 2010 (UTC)
Vilevile, ingefaa kujaza makala hiyo lakini tangu uanzishaji wake tarehe 21 Novemba 2009 hakuna. Isipopanuliwa, na ifutwe --Baba Tabita (majadiliano) 03:46, 30 Januari 2010 (UTC)
- Nakubali. Imeenda --Kipala (majadiliano) 11:13, 10 Februari 2010 (UTC)
Mtu huyo hajastahili kupata makala katika kamusi elezo. Kwa Kiingereza, makala ambazo zingestahili kuingizwa zimeelezwa hapa. Kwa sasa, makala hiyo ya Bw.Nassor ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 09:53, 2 Februari 2010 (UTC)
- Nakubali. Imeenda --Kipala (majadiliano) 11:13, 10 Februari 2010 (UTC)
Istilahi hiyo ni ya Kiingereza siyo ya Kiswahili. Tena haijaongezewa maneno hata kidogo. Na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 20:15, 4 Februari 2010 (UTC)
- Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 19:44, 6 Februari 2010 (UTC)
Makala hiyo haiongezi kitu kulingana na Alfabeti ya Kigiriki. Labda irejee kwa ile nyingine ila mimi sioni sababu ya kuingiza neno 'kamili' katika kichwa cha makala. Je, tofauti ni ipi? Machoni mwangu ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 20:21, 4 Februari 2010 (UTC)
- Nakubali. Imeenda --Kipala (majadiliano) 15:51, 9 Februari 2010 (UTC)
Kule kwa wikipedia ya Kiingereza makala hiyo imeshafutwa, wanadai habari hizo ni feki. Kwa vyovyote, jina lake la pili liandikwe na herufi kubwa. Kama hakuna ambaye angeweza kuleta habari thabiti kuhusu mtu huyo na kuonyesha kwamba kweli amestahili kutajwa katika kamusi elezo, na makala ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 20:27, 4 Februari 2010 (UTC)
- Nakubali. Inamhusu Mkenya anayejitokeza kama "nabii". maandishi yaonekana yamenakiliwa kutoka website yake ya kiingereza (au: lugha ya Kiskandinavia? "föreningar") na kupitishwa katika tafsiri ya mashine bila kusafishwa. Haifai kabisa. Imeenda --Kipala (majadiliano) 15:51, 9 Februari 2010 (UTC)
Makala duni kuhusu mtu ambaye labda hajastahili kutajwa katika kamusi elezo. Kama hakuna ambaye angeweza kuongeza habari, na makala ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 20:49, 4 Februari 2010 (UTC)
- Nakubali, ilikuwa jaribio sentensi isiyokamilika. Imeenda --Kipala (majadiliano) 15:51, 9 Februari 2010 (UTC)
Sentensi moja tu bila viungo vyovyote. Bila kupanuliwa, na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 20:51, 4 Februari 2010 (UTC)
- Nakubali. Imeenda --Kipala (majadiliano) 15:51, 9 Februari 2010 (UTC)
Haina yaliyomo tangu imeanzishwa tarehe 1 Desemba. Tena, nadhani iandikwe neno moja, yaani baruapepe (angalia makala ya Kiingereza kwa ajili ya kuanzisha makala hiyo). Kama isirejee kwa baruapepe, makala hii ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 10:28, 5 Februari 2010 (UTC)
- Nakubali. Imeenda. --Kipala (majadiliano) 15:51, 9 Februari 2010 (UTC)
Makala hiyo kweli ni kuhusu albamu Black & Blue, nayo makala ile iko tayari. Kwa vile mwandishi wa makala ni yuleyule, yaani Ndugu Abbas, makala hizo mbili ziko sawasawa, na moja ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 12:43, 5 Februari 2010 (UTC)
- Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 05:59, 10 Februari 2010 (UTC)
Sijui imeandikwa kwa lugha gani lakini si Kiswahili. Jaribio bovu la tafsiri ya kimachine? --Kipala (majadiliano) 15:39, 9 Februari 2010 (UTC)
- Ndiyo, wewe ni sahihi. Ni lazima ilifutwa. --MarsRover (majadiliano) 22:57, 9 Februari 2010 (UTC)
- Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 05:59, 10 Februari 2010 (UTC)
Makala hailingani na muundo wa kamusi.--Kipala (majadiliano) 19:34, 27 Novemba 2009 (UTC)
Kiswahili chake hakieleweki kabisa. Asili ilikuwa makala (sio nzuri kweli..) ya en:wiki iliyotafsiriwa kwa njia ya translate.google; inaonekana haikufanyiwa kazi ipasavyo. --Kipala (majadiliano) 17:09, 19 Desemba 2009 (UTC)
Isipoandikwa itafutwa. Hata kwa Kiingereza imeonywa na ufutaji. --Baba Tabita (majadiliano) 06:26, 10 Februari 2010 (UTC)
- Nakubali. Imeenda.--Kipala (majadiliano) 14:28, 16 Februari 2010 (UTC)
Isipoandikwa itafutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 06:26, 10 Februari 2010 (UTC)
- Nakubali. Kichwa cha maana lakini jinsi ilivyo uwezekano mkubwa itazuia kuandikwa makala kwa kufanya kiungo kionekane buluu. Imeenda.--Kipala (majadiliano) 14:28, 16 Februari 2010 (UTC)
Isipoandikwa itafutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 06:26, 10 Februari 2010 (UTC)
- Nakubali. Kichwa cha maana lakini jinsi ilivyo uwezekano mkubwa itazuia kuandikwa makala kwa kufanya kiungo kionekane buluu. Imeenda.--Kipala (majadiliano) 14:28, 16 Februari 2010 (UTC)
Isipoandikwa itafutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 06:26, 10 Februari 2010 (UTC)
- Nakubali. Kichwa cha maana lakini jinsi ilivyo uwezekano mkubwa itazuia kuandikwa makala kwa kufanya kiungo kionekane buluu. Imeenda.--Kipala (majadiliano) 14:28, 16 Februari 2010 (UTC)
Isipoandikwa itafutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 06:26, 10 Februari 2010 (UTC)
Isipoandikwa itafutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 06:26, 10 Februari 2010 (UTC)
- Nakubali. Imeenda.--Kipala (majadiliano) 14:28, 16 Februari 2010 (UTC)
Isipoandikwa itafutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 06:26, 10 Februari 2010 (UTC)
- Nakubali. Imeenda.--Kipala (majadiliano) 14:28, 16 Februari 2010 (UTC)
Isipoandikwa itafutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 06:26, 10 Februari 2010 (UTC)
- Nakubali. Kichwa cha maana lakini jinsi ilivyo uwezekano mkubwa itazuia kuandikwa makala kwa kufanya kiungo kionekane buluu. Imeenda.--Kipala (majadiliano) 14:28, 16 Februari 2010 (UTC)
Haina habari. Ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 14:30, 10 Februari 2010 (UTC)
- Nakubali. Imeenda.--Kipala (majadiliano) 14:28, 16 Februari 2010 (UTC)
Siyo makala ifaayo kwa kamusi elezo. Ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 14:30, 10 Februari 2010 (UTC)
- Nakubali. Imeenda.--Kipala (majadiliano) 14:28, 16 Februari 2010 (UTC)
Haina habari. Ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 14:40, 10 Februari 2010 (UTC)
- Nakubali. Kichwa cha maana lakini jinsi ilivyo uwezekano mkubwa itazuia kuandikwa makala kwa kufanya kiungo kionekane buluu. Imeenda.--Kipala (majadiliano) 14:28, 16 Februari 2010 (UTC)
Haina habari. Ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 14:58, 10 Februari 2010 (UTC)
- Nakubali. Kichwa cha maana lakini jinsi ilivyo uwezekano mkubwa itazuia kuandikwa makala kwa kufanya kiungo kionekane buluu. Imeenda.--Kipala (majadiliano) 14:28, 16 Februari 2010 (UTC)
Sentensi moja tu isiyofaa kwa kamusi elezo. Ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 14:58, 10 Februari 2010 (UTC)
- Nakubali. Imeenda.--Kipala (majadiliano) 14:28, 16 Februari 2010 (UTC)
Sentensi moja tu isiyofaa kwa kamusi elezo. Ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 14:58, 10 Februari 2010 (UTC)
- Nakubali. Imeenda.--Kipala (majadiliano) 14:28, 16 Februari 2010 (UTC)
Haina habari. Ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 15:10, 10 Februari 2010 (UTC)
- Nakubali. Kichwa cha maana lakini jinsi ilivyo uwezekano mkubwa itazuia kuandikwa makala kwa kufanya kiungo kionekane buluu. Imeenda.--Kipala (majadiliano) 14:28, 16 Februari 2010 (UTC)
Hii ni insha isiyofaa kwa kamusi elezo. Kwa vyovyote, ni kuhusu soko la simu ya mkononi nchini Tanzania, kwa hiyo hata kichwa chake hakifai. Isipobadilishwa kufuatana na kanuni za kamusi elezo, na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 15:10, 10 Februari 2010 (UTC)
- Nakubali. Imeenda.--Kipala (majadiliano) 14:28, 16 Februari 2010 (UTC)
Haina habari. Ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 17:31, 12 Februari 2010 (UTC)
- Siwezi kuifuta maana jina lake linazuiliwa hapa kwetu na filta ya serikali. Basi afute mwingie! --Kipala (majadiliano) 14:04, 16 Februari 2010 (UTC)
- Haya, imeenda. --Baba Tabita (majadiliano) 14:19, 16 Februari 2010 (UTC)
Haina habari. Isipoandikwa, na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 17:31, 12 Februari 2010 (UTC)
- Nakubali. Kichwa cha maana lakini jinsi ilivyo uwezekano mkubwa itazuia kuandikwa makala kwa kufanya kiungo kionekane buluu. Imeenda.--Kipala (majadiliano) 14:28, 16 Februari 2010 (UTC)
Haina habari. Tena haileti maana (angalao haileti maana kwangu). Ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 14:30, 16 Februari 2010 (UTC)
- Nakubali. Imeenda.--Kipala (majadiliano) 18:04, 18 Februari 2010 (UTC)
Haina kitu. Ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 15:06, 16 Februari 2010 (UTC)
- Nakubali. Imeenda.--Kipala (majadiliano) 18:04, 18 Februari 2010 (UTC)
Haina kitu. Ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 15:06, 16 Februari 2010 (UTC)
- Nakubali. Imeenda.--Kipala (majadiliano) 18:04, 18 Februari 2010 (UTC)
Imefutwa --Kipala (majadiliano) 20:35, 21 Februari 2010 (UTC)
Inaonekana pendekezo lilikosea kutaja ukurasa wa majadiliano; makala iko. Inabaki. --Kipala (majadiliano) 20:35, 21 Februari 2010 (UTC)
Imefutwa --Kipala (majadiliano) 20:35, 21 Februari 2010 (UTC)
Inaonekana ni tafsiri ya makala ya gazeti au insha si makala ya kamusi. Sioni habari za ziada kulingana na bangi. Iende. --Kipala (majadiliano) 18:01, 18 Februari 2010 (UTC)
- Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 10:12, 5 Aprili 2010 (UTC)
Mtayarishaji wa filamu - IBAKI!
[hariri chanzo]Haina habari yoyote. Kama hakuna atakayeingiza mambo, k.m. kutoka makala ya Kiingereza, na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 16:05, 5 Aprili 2010 (UTC)
- Nitaishughulikia makala hii, lakini nitahitaji ushirikiano, hasa wa Muddyb. --Coolsam726 (majadiliano) 17:09, 5 Aprili 2010 (UTC)
- Asanteni sana. Naona kazi pamoja na Muddyb imeshaanza. Makala imeendelezwa na ibaki. --Baba Tabita (majadiliano) 08:56, 6 Aprili 2010 (UTC)
Haina habari yoyote. Kama hakuna atakayeingiza mambo, na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 11:18, 5 Aprili 2010 (UTC)
- Hakuna aifanyiaye kazi kwa wiki mbili. Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 11:22, 19 Aprili 2010 (UTC)
Haina habari yoyote. Kama hakuna atakayeingiza mambo, na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 11:38, 5 Aprili 2010 (UTC)
- Hakuna aifanyiaye kazi kwa wiki mbili. Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 11:22, 19 Aprili 2010 (UTC)
Haina habari yoyote. Kama hakuna atakayeingiza mambo, na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 12:02, 5 Aprili 2010 (UTC)
- Hakuna aifanyiaye kazi kwa wiki mbili. Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 11:22, 19 Aprili 2010 (UTC)
Wala wanadamu wa Tsavo - IBAKI!
[hariri chanzo]Haina habari yoyote. Kama hakuna atakayeingiza mambo, k.m. kutoka makala ya Kiingereza, na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 12:15, 5 Aprili 2010 (UTC)
- Nitaihariri makala hii. Coolsam726 (majadiliano) 17:12, 5 Aprili 2010 (UTC)
- Asante, Coolsam, kwa kuitafsiri kutoka Kiingereza! --Baba Tabita (majadiliano) 09:52, 14 Aprili 2010 (UTC)
Chanzo au asili ya neno hili wapi? Halipo mtandaoni wala silipati katika kamusi yoyote, hata katika kamusi za isimu. Tena, "mofimu inayosababisha ukanushi katika kitenzi" ni kikanushi. Bila marejeo yanayoonyesha kwamba neno hilo kweli lipo, na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 13:26, 5 Aprili 2010 (UTC)
- Hakuna aifanyiaye kazi kwa wiki mbili. Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 11:24, 19 Aprili 2010 (UTC)
Haina habari yoyote. Kama hakuna atakayeingiza mambo, k.m. kutoka makala ya Kiingereza, na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 13:29, 5 Aprili 2010 (UTC)
- Hakuna aifanyiaye kazi kwa wiki mbili. Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 11:24, 19 Aprili 2010 (UTC)
Mila na tamaduni idakho - IBAKI!
[hariri chanzo]Kichwa hakifai. Bora makala iandikwe chini ya Waidakho. Tena, haina habari yoyote bado. Kama hakuna atakayeingiza mambo, k.m. kutoka makala ya Kiingereza, na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 13:33, 5 Aprili 2010 (UTC)
- Makala haya nitayaangalia kaka hivi karibuni,tafadhali yasifutwe.Limoke oscar (majadiliano) 13:27, 6 Aprili 2010 (UTC)
- Asante, Limoke, kwa kazi yako kwenye ukurasa wa Waidakho. Faili hii sasa nimeirejesha kwa makala uliyoiandika. --Baba Tabita (majadiliano) 09:52, 14 Aprili 2010 (UTC)
Huyu bwana hajastahili kuingizwa kwenye kamusi elezo. Kwa maelezo ya "kustahili kuingizwa" kwa Kiingereza, angalia hapa. --Baba Tabita (majadiliano) 07:08, 19 Aprili 2010 (UTC)
- Maajabu! Sijui hajui kama Wikipedia haiandiki habari za watu wa kawaida? Tumpe pole. Baba T, peleka machinjioni makala hii.--MwanaharakatiLonga 07:23, 19 Aprili 2010 (UTC)
- Imechinjwa. --Baba Tabita (majadiliano) 08:01, 19 Aprili 2010 (UTC)
Hakuna sheria za baraza hilo, ni maazimio tu, angalia makala ya Kiingereza. --Baba Tabita (majadiliano) 10:41, 5 Aprili 2010 (UTC)
- Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 06:01, 27 Aprili 2010 (UTC)
Haina habari yoyote. Kama hakuna atakayeingiza mambo, k.m. kutoka makala ya Kiingereza, na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 10:43, 5 Aprili 2010 (UTC)
- Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 06:01, 27 Aprili 2010 (UTC)
Haina habari yoyote. Kama hakuna atakayeingiza mambo, k.m. kutoka makala ya Kiingereza, na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 13:16, 5 Aprili 2010 (UTC)
- Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 06:01, 27 Aprili 2010 (UTC)
Habari hizo zote tayari zimo katika makala ya Tarakilishi. Basi nakala chini ya kichwa hicho kisichofaa ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 08:01, 19 Aprili 2010 (UTC)
- Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 06:01, 27 Aprili 2010 (UTC)
Na hii tena vilevile, nakala nyingine chini ya kichwa kisichofaa. Ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 08:05, 19 Aprili 2010 (UTC)
- Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 06:01, 27 Aprili 2010 (UTC)
Ni Kiingereza tu, tena ni tangazo la biashara. Haifai kwa kamusi elezo. Ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 08:50, 19 Aprili 2010 (UTC)
- Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 06:01, 27 Aprili 2010 (UTC)
Kuhariri Mchango wa tume ya Ominde (1964),Mackay (1981) na Koech katika kustawisha lugha ya Kiswahili nchini Kenya.
[hariri chanzo]Ni insha, siyo makala ifaayo kwa kamusi elezo. Basi, ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 09:21, 19 Aprili 2010 (UTC)
- Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 06:01, 27 Aprili 2010 (UTC)
Haina hata neno moja. Kama hakuna ambaye angeweza kuiandika, na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 10:02, 19 Aprili 2010 (UTC)
- Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 06:01, 27 Aprili 2010 (UTC)
Haina habari yoyote. Kama hakuna atakayeingiza mambo, k.m. kutoka makala ya Kiingereza, na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 10:24, 5 Aprili 2010 (UTC)
Haina habari yoyote. Kama hakuna atakayeingiza mambo, k.m. kutoka makala ya Kiingereza, na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 10:28, 5 Aprili 2010 (UTC)
Rais wa Afrika Kusini imefutwa
[hariri chanzo]Haina habari yoyote. Kama hakuna atakayeingiza mambo, k.m. kutoka makala ya Kiingereza, na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 12:13, 5 Aprili 2010 (UTC)
- Ninaishughulikia makala hii Coolsam726 (majadiliano) 17:06, 5 Aprili 2010 (UTC)
Halijoto inabaki - tayari imepanuliwa
[hariri chanzo]Haina habari yoyote. Kama hakuna atakayeingiza mambo, k.m. kutoka makala ya Kiingereza, na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 13:16, 5 Aprili 2010 (UTC)
Kubadilika wa viumbe hai inabaki kama kielekezo
[hariri chanzo]Habari zilizomo hazifai kwa kamusi elezo. Kwa vyovyote, hakuna marejeo wala viungo ambavyo vingethibitisha yaliyomo. Tena, kichwa kiwe "Mageuko ya spishi" - angalia majadiliano ya makala. Mimi naona ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 09:31, 19 Aprili 2010 (UTC)
Madesa imefutwa
[hariri chanzo]Machoni mwangu haina umuhimu wa kutosha ili kubaki katika kamusi elezo. Naona ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 09:38, 19 Aprili 2010 (UTC)
Majina ya wazigua imefutwa
[hariri chanzo]Makala hii isipopanuliwa na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 09:43, 19 Aprili 2010 (UTC)
Watoto wa mitaani imefutwa
[hariri chanzo]Makala hii ilivyo haifai kwa kamusi elezo. Sijui la kufanya nayo. Labda iandikwe upya kufuatana na makala ya Kiingereza. La sivyo, na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 11:20, 19 Aprili 2010 (UTC)
Uhusiano wa lugha na utamaduni imefutwa
[hariri chanzo]Yaliyomo haina maana. Ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 12:31, 22 Aprili 2010 (UTC)
Historia ya mchezo wa soka imefutwa
[hariri chanzo]Sentensi moja tu isiyofaa kwa kamusi elezo. Isipopanuliwa, k.m. kutokana na makala ya Kiingereza, na ifutwe. Kwa vyovyote ingekuwa vizuri zaidi kusogeza makala hii kwenda Historia ya mpira wa miguu. --Baba Tabita (majadiliano) 10:17, 7 Mei 2010 (UTC)
Uongezekaji Wa Joto Ulimwenguni imefutwa
[hariri chanzo]Napendekeza kufuta makala hii. Utafsiri ni mbaya, kuipanga upya ni kazi kubwa mno, na kichwa kipo tayari (kupanda kwa halijoto duniani). Au yupo anayetaka kufanya kazi hii?? --Kipala (majadiliano) 08:23, 27 Mei 2010 (UTC)
- Nadhani ni yale matunda ya bandia ya google translator na mipango ya kuitetea! Oliver kachomoa ombi jipya kwa matatizo kama haya. Simuoni wa kuirekebisha ukishindwa wewe. Chukua hatua inayofaa ikiwezekana!--MwanaharakatiLonga 10:18, 27 Mei 2010 (UTC)
Je, huyu mzee kweli anastahili kupata makala katika kamusi elezo? Isipopatikana habari zionyeshazo umaarufu wake, na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 10:54, 19 Aprili 2010 (UTC)
- Imefanyika. Haijulikani yeye ni nani wale kitu gani. Si mtunzi, mwandishi, mwigizaji, mwanasiasa au aje? Amekwenda na maji!--MwanaharakatiLonga 15:13, 11 Juni 2010 (UTC)
Makala hii haileti maana; hata kwa Kiingereza ni mbegu. Viungo vingi ni vitupu, na hakuna jamii wala viungo vya maana vingine. --Baba Tabita (majadiliano) 13:43, 31 Mei 2010 (UTC)
- Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 13:01, 11 Juni 2010 (UTC)
Kichwa batili. Yaliyomo yaunganishwe na Julius Nyerere, basi ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 13:50, 31 Mei 2010 (UTC)
- Imefanyika. Habari za kujirudia na makala yenye kueleza habari kama hizi ipo (Nyerere). Tena hii haina habari za kujitosheleza!--MwanaharakatiLonga 15:13, 11 Juni 2010 (UTC)
Kichwa batili. Yaliyomo yaunganishwe na Mkoa wa Mwanza, basi ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 13:52, 31 Mei 2010 (UTC)
- Imefanyika. Kweli makala ya Mkoa wa Mwanza ipo! Imekwenda na maji!--MwanaharakatiLonga 15:13, 11 Juni 2010 (UTC)
Makala hii haifai kwa kamusi elezo. Tena ina kosa kwenye kichwa ('sheri' badala ya 'sheria'). Basi ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 22:00, 11 Juni 2010 (UTC)
- Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 13:46, 15 Juni 2010 (UTC)
Makala hii inaelekea viungo vitupu tu. Tena, interwiki zake haziungi na makala zinazotofautisha maana bali makala za mwimbaji fulani ambayo haijaandikwa kwa Kiswahili. Isiporekebishwa, na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 22:12, 11 Juni 2010 (UTC)
Ingawa makala ingestahili kuwepo bado haijajazwa habari yoyote. Isipopanuliwa na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 06:07, 12 Juni 2010 (UTC)
Makala hii haina kitu. Isipopanuliwa na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 06:10, 12 Juni 2010 (UTC)
Makala hii ingefaa kwa sw.wiktionary.org siyo kwa kamusi elezo lakini. Na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 06:12, 12 Juni 2010 (UTC)
Tumbi IBAKI!!!
[hariri chanzo]Ina viungo vitupu tu. Kama hakuna atakayeandika makala kuhusu kata zirejelewazo na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 06:18, 12 Juni 2010 (UTC)
- (ilikuwa kazi tu ya kusahihisha tahajia ya viungo) --Kipala (majadiliano) 11:03, 12 Juni 2010 (UTC)
Sioni sababu mtu huyu astahili kupata makala katika kamusi elezo. Asipofahamika nje ya ndugu, marafiki na wanafunzi wake, na makala yake ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 06:30, 12 Juni 2010 (UTC)
Arusha Times IBAKI!!!
[hariri chanzo]Ingawa makala ingestahili kuwepo bado haijajazwa habari yoyote. Isipopanuliwa na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 06:31, 12 Juni 2010 (UTC)
Haina kitu. Tena, inaonekana kama iwe jamii badala ya makala. Isipopanuliwa wala kutafsiriwa kutoka Kiingereza, na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 16:36, 11 Juni 2010 (UTC)
- Imefutwa.
Sioni mtu huyu ana umaarufu wa kutosha ili astahili makala ya kamusi elezo. Kama hakuna habari ambazo zingeonyesha umaarufu wake, na makala ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 06:57, 14 Juni 2010 (UTC)
- Imefutwa.
Makala ni kwa Kiingereza siyo kwa Kiswahili. Tena, sijamuona huyo mtu mtandaoni wala mahali pengine kama kweli ana umaarufu wa kutosha ili astahili makala kwenye kamusi elezo. La sivyo na ifutwe, --Baba Tabita (majadiliano) 13:45, 15 Juni 2010 (UTC)
- Imefutwa.
Makala hii haifai kwa kamusi elezo, ni kama mbegu ya insha ya kifalsafa. Machoni mwangu na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 22:13, 21 Juni 2010 (UTC)
- Imefutwa.
Ina viungo vitupu tu. Kama hakuna atakayeandika makala kuhusu wale watu warejelewao na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 06:19, 12 Juni 2010 (UTC)
- Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 10:29, 5 Agosti 2010 (UTC)
Makala hii inaonekana kama imetafsiriwa vibaya kwa mashine. Kiswahili chake hakieleweki. Tena, haina viungo wala jamii za kawaida. Isiporekebishwa na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 12:06, 12 Juni 2010 (UTC)
- Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 10:29, 5 Agosti 2010 (UTC)
Hakuna viungo vyovyote, maelezo hayaridhishi.--Kipala (majadiliano) 14:14, 4 Julai 2010 (UTC)
- Imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 10:29, 5 Agosti 2010 (UTC)
Imependekezwa ifutwe na mtumiaji asiyejisajili. Hata hivyo, makala haijatafsiriwa vizuri na isiporekebishwa nami naomba ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 10:37, 5 Agosti 2010 (UTC)
- Imefanyika.--MwanaharakatiLonga 09:55, 13 Agosti 2010 (UTC)
Hii ni maoni siyo makala inayofaa kwa kamusi elezo. Na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 09:37, 7 Agosti 2010 (UTC)
- Imefanyika.--MwanaharakatiLonga 09:55, 13 Agosti 2010 (UTC)
Haijaingizwa habari za maana. Isipopanuliwa na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 09:46, 7 Agosti 2010 (UTC)
- Imefanyika.--MwanaharakatiLonga 09:55, 13 Agosti 2010 (UTC)
Makala hii ina sentensi moja tu iliyotafsiriwa vibaya. Tena haina viungo wala jamii. Isiporekebishwa, na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 10:56, 9 Agosti 2010 (UTC)
- Imefanyika.--MwanaharakatiLonga 09:55, 13 Agosti 2010 (UTC)
Makala hii imetafsiriwa vibaya. Tena haina viungo wala jamii. Isiporekebishwa, na ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 10:58, 9 Agosti 2010 (UTC)
- Imefanyika.--MwanaharakatiLonga 09:55, 13 Agosti 2010 (UTC)
Mbegha - IBAKI!
[hariri chanzo]Haieleweki ni mnyama gani, makala haifai. Yupo mwenye habari juu ya Mbegha? Menginevyo ifutwe. Kipala (majadiliano) 11:42, 15 Septemba 2010 (UTC)
- http://www.answers.com/topic/mbegha-s-transformation --CGN2010 (majadiliano) 11:47, 15 Septemba 2010 (UTC)
- i have replaced the delete by a unreferenced. The author is A) new: they should be given a chance to get accustomed to wikipedia and B) he is mixing folklore with history for an otherwise very relevant article. Please lets continue the discussion on the articles talk page. --CGN2010 (majadiliano) 20:43, 15 Septemba 2010 (UTC)
- http://www.answers.com/topic/mbegha-s-transformation --CGN2010 (majadiliano) 11:47, 15 Septemba 2010 (UTC)
Probably the same guy. Makala inakosa maelezo yanayotakiwa kulingana na kamusi elezo. Iboreshwe na kupelekwa kwenye hali ya kitaalamu kiasi au ifutwe. Kama mwanzilishaji anaamini kuwepo kwa majini, mapepo n.k. sharti ajue kwa nini watu wengine hawaamini hasa wataalamu hawakubali hoja hili, sharti aweze kutaja maoni mengine na sababu zao na kurejea majadiliano yaliyopo katika swali hili Kipala (majadiliano) 08:16, 16 Septemba 2010 (UTC)
Imependekezwa ifutwe na mtumiaji asiyejisajili. Hata hivyo, makala haijatafsiriwa vizuri na isiporekebishwa nami naomba ifutwe. --Baba Tabita (majadiliano) 10:37, 5 Agosti 2010 (UTC)
- Kwa vile hakuna aliyeirekebisha vya kutosha, sasa imefutwa. --Baba Tabita (majadiliano) 14:56, 25 Oktoba 2010 (UTC)