Uwanja wa Dhambi
Makala haina vyanzo vya kutosha
Makala (au sehemu ifuatayo ya makala) inatoa habari bila kuonyesha vyanzo au uthibitisho wowote.
|
Makala hii au sehemu ya makala hii inahitaji masahihisho kwa upande mmoja wa zifuatazo:
|
Maelezo ya sinema kwa ufupi
[hariri | hariri chanzo]Sinema inaanza kwa kumuonyesha mwanamke anayeitwa Mama Shubiri akipanganga vitu vyake vya kichawi katika mkeka. Kamera vitu ni vyungu vitatu, usinga, vibuyu, dawa za unga, mayai yaliyoandikwa, glass, chupa zenye marashi, ungo ulijaa mjani, vitamba vyekundu vimetandikwa, kisu chenye ncha kali. Pia inaonyesha moto unaowaka. Nje barabarani kwa mbali waonekana wenzake wakiwa wamevaa mavazi mekundu na meusi, wakitokea makaburini huku wakiwa wamebeba maiti ya mwili wa Mwanaume.(ambaye ni Mzee Joshua) Wanaonekana wakitembea huku wakiimba wimbo wa kichawi. (Tumemwita amekuja, mwana wa binadamu.Eeee amekuja. Mwana wa bindamu.Chakula chetu nyama. Kinywaji chetu damu.) Mama Shubiri anasikia sauti ya wenzake. Ananyanyuka na kuanza kucheza huku akiimba. Wanaonekana wamefika na kuiweka maiti juu ya mkeka karibu na chungu kikubwa. Mama Shubiri anamchoma na kisu tumboni na kuanza kunywa damu. Wenzake nao wanakunywa damu hiyo. Kutokana na kupenda kufanya vitendo vya kichawi, anamua kumfanya mumewe kuwa ndondocha na kumtumisha kama mfanyakazi wake wa ndani. Anamgeuza mumewe kama kistuli cha kuwekea miguu. Anamsaidia binti yake Shubiri kuchukua mwanaume wa msichana anayeitwa Jamila. Wakati binti huyo anapokuja kumtaka mtoto wa Mama Shubiri kumwachia mume wake. Mama Shubiri anaamua kumfanya ndondocha kwa ajili ya kumkomoa binti huyo na mumewe anachukuliwa na mtoto wake Shubiri. Kama haitoshi Mama Shubiri anataka kumuua mtoto wake wa kufikia.Anashindwa kufanya hivyo kutokana na nguvu za ajabu alizopewa na Malaika. Ikimbukwe kuwa majirani zake wengi amewaingilia kiuchawi nyakati za usiku na kuwafanyia vitendo vya kichawi. Amemuingilia mpaka Mganga wa kienyeji na kumchukua kumfanya ndondocha. Hayo ni baadhi ya matukio yaliyokuwa katika sinema hiyo ya uwanja wa dhambi. Ni dhambi kweli zilizofanyika katika sinema hiyo.
Washiriki wakuu
[hariri | hariri chanzo]- 1 Aisha Chanzi ( Mama Shubiri )
- 2 Mwajuma Abdul (Maimuna )
- 3 Stella Bartazali ( Shubiri )
- 4 Fatuma Mwinchumu( Mama Rose )
- 5 Zainabu Mbavumbili( Mama Lulu )
Washiriki wengine
[hariri | hariri chanzo]- 6 Rose John ( Jamila]] )
- 7 Omari Pembe ( Ben )
- 8 Fide Njokamanl (Mzee Kashata )
- 9 Joseph Micheal ( Mganga wa kienyeji )
Watengenezaji
[hariri | hariri chanzo]- 1 Mtunzi ( Haji Dilunga )
- 2 Mtayarishaji mkuu ( Faraji Mohamed )
- 3 Mtayarishaji Msaidizi ( Haji Dilkunga )
- 4 Mhariri ( Khalifan Mwinshehe )
- 5 Muongozaji Mkuu( Haji Dilunga )
- 6 Muongozaji Msaidizi ( Salum Karanda )
- 7 Muziki ( Elisha Mabinda )
- 8 Msambazaji( Kampuni ya Wananchi wote )
- 9 Imetengenezwa ( Mwaka 2006 )