Haji Dilunga
Haji Dilunga | |
---|---|
Amezaliwa | Haji Dilunga 19 Machi 1973 Tanga Tanzania |
Kazi yake | Mwongozaji wa filamu Mtunzi na Mwandishi wa Script Mwandishi wa habari Mwandishi wa vitabu Mtayarishaji wa sinema |
Ndoa | Ana mke na watoto wawili |
Haji Dilunga (amezaliwa tar. 19 Machi 1973) ni mwongozaji na pia mtunzi wa filamu kutoka nchini Tanzania. Yeye ni miongoni mwa watayarishaji vijana wanaochipukia katika fani ya utengenezaji wa filamu za Kitanzania kwa kutayarisha filamu ya Ngome ya Mwanamalundi.
Mtayarishaji mkuu wa filamu hiyo alikuwa Ben Mtobwa na filam liongozwa na Hammie Rajabu. Baada ya hapo, alitayarisha sinema ya Lazima ufe Joram. Alianzisha kundi la sanaa linaloitwa Alwatan na kutayarisha filamu nyingine nyingi na kuziongoza mwenyewe.
Haji Dilunga anatoka katika ukoo wa wenye vipaji vingi kama wachezaji mpira na waigizaji. Mdogo wake ni Mwajuma Abdul, naye ni mwigizaji aliyejipatia umaarufu mkubwa zaidi baada ya kushiriki katika tamthilia ya Hukumu ya Tunu.
Filamu ambazo amezitengeneza hadi sasa ni, Uwanja wa Dhambi, I love You, Picnic, Bunge la Bachawi (Part I & II), Popobawa, Zindiko.Mbali ya utayarishaji na uongozaji wa sinema ni mwandishi wa habari,anayependa kuandika habari za burudani, utamaduni, sanaa, muziki, michezo, mila na jadi.
Kwa vile na penda kudadaisi vitu na kufanya uchunguzi,amefanikiwa kugundua mambo mbali mbali ya maisha na tabia za watu na hatimaye kuandika vitabu vya watoto vinavyotumika shuleni kama vitabu vya ziada ambavyo ni Sungura na kassa, Jamila na pete ya ajabu. Vinatumika katika shule za msingi. Pia ameandika vitabu vya mahusiano kama vile Penzi Starehe na Mapenzi ya Ajabu.
Baadhi ya ya magazeti aliyowahi kuandikia ni pamoja na Motomoto,Tanganyika Leo,Bahari,Baraza,Democrat, Majira, Dar Leo, Jitambue, Tanzania leo kwa nyakati tofauti.Na sasa ni mhariri wa habari wa gazeti la Mtandao.
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Tovuti Rasmi ya Haji Dilunga Ilihifadhiwa 4 Februari 2006 kwenye Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Haji Dilunga kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |