Mwajuma Abdul

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Mwajuma Abdul (Dar es Salaam, Tanzania, 1977 - 28 Juni 2016, ) alikuwa muigizaji wa vipindi vya televisheni na filamu nchini Tanzania.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Mwajuma Abdul au Maimuna alizaliwa mwaka 1977 jijini Dar es Salaam, alipata elimu ya awali shule ya msingi Mjimwema. Mwajuma alipata elimu ya msingi katika shule ya Mjimwema na kujiunga shule ya sekondari ya bweni ya Iringa Girls iliyopo Iringa; baada ya hapo alijiunga na masomo ya ukatibu mukhatasi.

Baada ya hapo alijiunga na kikundi cha sanaa cha The Lighters kilichokuwa na makao makuu yake Kimara. Alijipatia umaarufu mkubwa katika sinema ya Uwanja wa Dhambi, Mwajuma Abdul a.k.a Maimuna ameibuka tena katika filamu nyingine ya kutisha inayoitwa Picnic. Kwa mujibu wa maelezo yake, amesema nafasi hiyo ameipata baada ya kuonekana ana kiwango kikubwa cha uigizaji, hasa baada ya kuimudu nafasi yake aliyocheza ya kupambana na mchawi Mama Shubiri katika sinema ya Uwanja wa dhambi. Katika sinema ya Picnic amecheza kwa kutumia jina la Dora, Katika sinema hiyo anacheza kama Mzimu unaokuja kulipa kisasi kwa kitendo alichofanyiwa na vijana wenzake. Mzimu wa Dora unawatokea vijana hao waliokwenda Picnic Bagamoyo wakitokea Dar es Salaam, wakiwa na furaha ya kuona magofu ya kaole na kupata historia ya mji huo, wanatokewa na mzimu wa Dora na kuanza kuua mmoja baada ya mwingine. Furaha ya Picnic inageuka na kuwa majonzi makubwa.

Kuhusu fani ya uigizaji, alianza toka alivyokuwa shule ya msingi. Na hata baada ya kumaliza masomo, aliamua kuendelea na sanaa kwa kujiunga na kikundi cha The Lighters kilichokuwa na Maskani yake Kimara. Pia, anashiriki katika mchezo wa redio wa Twende na wakati unarushwa na kituo cha redio Tanzania. Amesema baada ya kutoka Lighters aliamua kujiunga na Kaole kwa ajili ya kufanya sanaa za kwenye Luninga. Alijitoa Kaole na kujiunga na kundi la Alwatan Artist Theatre. Alitaja baadhi ya Sinema alizocheza ni pamoja na Joram Lazima Ufe, ni kitabu kilichoandikwa na mwandishi maarufu barani Afrika, Ben Mtobwa. Kitabu hicho kimejipatia umaarufu mkubwa ndani ya nchi na nje ya mipaka ya Tanzania. Sinema nyingine alizocheza ni Uwanja wa Dhambi. Katika filamu hiyo amecheza kama Maimuna. Sinema ni I love you amecheza kwa jina Rose, Husda amecheza kwa jina la Rose, nyingine Zindiko amecheza kwa jina la Amanda. Kuhusu wa wasanii wa Kibongo anavutiwa na Anne Mwampamba na Mikala. Wasanii wa nje wanamvutia ni Bruce Lee, Anjela Mau na Genenve Nnanji. Pia ameshiriki katika tamthilia inayotengenezwa na Benchmak inayoitwa hukumu ya Tunu itanayorushwa na ITV.