Anne Mwampamba
Anne Mwampamba Miaka yake ni 34, Elimu ya sekondari Meta, Mbeya Ni Mkristo, Mfanyakazi wa kampuni ya City Elevator ya Jijini Dar es Salaam, Tanzania. Ni muigizaji wa kikundi cha sanaa cha Alwatan kinachotngeneza filamu za kibongo nchini Tanzania.Ana mtoto mmoja anayeitwa Blendina
Sanaa alipenda toka alivyokuwa mdogo, katika malengo yake ilikuwa ni kuja kuwa msanii, aliangaika kutafuta vikundi mbali mbali vya kujiunga. Alijiunga na kikundi cha Brown eyes alifanikiwa kucheza sinema ya vichekesho inayoitwa Mzee Chabo. Alicheza nafasi ya msichana anayechunguliwa na Mzee Majuto. Baada ya kujiunga na kundi la Alwatan amefanikiwa kucheza sinema ya Bunge la Wachawi. Katika sinema amecheza kama mwanamke anayechukuliwa mume wake na mwanamke mchawi. Kuhusu wasanii wa kibongo anavutia na Mwajuma Abdul a.k.a Maimuna naNdumbagwe Misayo a.k.a Tea. Kwa upande madirector (Waongozaji) anavutia na Haji Dilunga . Amesema ni muongozaji asiyekuwa na matusi wala kashfa ukilinganisha na wengine. Kuhusu wasanii wa nje ya Bongo anavutiwa na Genenve Nnanji na Ramsel Noah Anachukia majungu na watu wanaopenda kujikweza.
Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Anne Mwampamba kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |