Majadiliano:Uwanja wa Dhambi
Salaam, Wanawikipedia. Mtanisamehe kwa kuziweka kitangazo cha ufutaji juu ya makala hizi mbili. Masuala ya kutaka kuandika makala za filamu yanahitaji mambo mengi mno kiasi kwamba si rahisi kwa filamu za Tanzania kuweza kuandikwa katika Wikipedia - ilhali wao wenyewe hawataki kudhihirisha hali halisi ya washiriki ama wajenzi wa filamu. Mambo hay ni pamoja na kuweka kitu kama:
- Washiriki
- Wahariri
- Waongozaji/mwongozaji
- Wasambazaji
- Watayarishaji
Na mengine mengi tu yanatakiwa yawepo kwenye filamu. Makala haijataja filamu imetolewa mwaka ama kutengenezwa. Makala haijataja nani mwigizaji kiongozi wa filamu hii. Hivyo ninapendekeza makala zote zifutwe, maanake hatuwezi kuandika vitu ambavyo haviendani na mwenendo wa kamusi elezo ya Wiki vile inavyosema. Wenu mtiifu,--Mwanaharakati (Longa) 05:54, 16 Februari 2009 (UTC)
- Nakubali jinsi ilivyo haifai kabisa. Kama hakuna anayeweza kuibadilisha kuwa makala halali basi ifutwe hata nikiona hasara ya kufuta makala juu ya filamu ya Kitanzania. Lakini si vema kama makala juu ya filamu ya Kitanzania ni bovu na zile juu ya filamu za nje ni safi. Heri iende. Tusubiri wiki moja. --Kipala (majadiliano) 13:53, 16 Februari 2009 (UTC)
- Kuna mtu kaweka maelezo yote yale katika ukurasa husika, lakini kafuta kile kitangazo cha "futa" halafu kaweka maelezo mengine bila kuancha maelezo yoyote kwenye ukurasa wa majadiliano. Nitajaribu kuiweka sawa, nikishindwa, basi kisu kipite!--Mwanaharakati (Longa) 12:51, 20 Februari 2009 (UTC)