Bongo Records

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bongo Records
Imeanzishwa 1995
Mwanzilishi P Funk Majani
Ilivyo sasa Bado inafanya kazi
Aina za muziki Hip hop
Bongo Flava
Dansi
Nchi Tanzania
Mahala Kinondoni, Dar es Salaam

Bongo Records ni studio ya kurekodia muziki nchini Tanzania. Studio inamilikiwa na mtayarishaji wa muziki wa hip hop na Bongo Flava P Funk Majani. Studio ilianzishwa mnamo mwaka wa 1995 ikiwa na ya wasanii wachache.

Pindi ilipoanzishwa haikuwa na umaarufu kutokana na mandhari ya muziki unaopigwa huko ulikuwa tofauti kidogo na mazoea ya Watanzania. Taratibu ilianza kupata heshima na hata kujulikana zaidi katika jiji la Dar es Salaam na kunako miaka ya 2000 studio ilivuma na kuthubutu kuzishinda hata studio nyingine zilizopo katika mji huo.

Bongo records ina historia ndefu ya kufanya kazi na wanamuziki wengi wa Bongo Flava kama Juma Nature, Cpwaa, Jay Moe, Mangwea na Joe Makini.

Mwaka 2019 Bongo Records imeingia mkataba na Anaieitwa Rapcha, msanii mdogo anayechipukia katika muziki wa Afrika Mashariki na anatabiriwa kufanya makubwa katika sanaa yake.

Tarehe 20 Desemba 2019 Pfunk Majani aliachia wimbo chini ya Bongo records unaoitwa Moto Unawaka akimshirikisha Rapcha, TkiLLA na msamiati.

Tarehe 10 September 2021 Bongo records imetambulisha album ya kwanza ya Rapcha inayoitwa Wanangu99 ikihusisha hits kama “Lissa” ambayo ina watazamaji zaidi ya milioni kwenye mtandao wa youtube mpaka sasa.

Makala hii kuhusu mambo ya muziki bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Bongo Records kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.