Nenda kwa yaliyomo

P. Funk

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka P Funk)
Paul Majani

Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Paul Matthysse
Pia anajulikana kama P Funk, Majani, Kinywele Kimoja, Mdachi nk.
Asili yake Tanzania
Aina ya muziki Hip Hop na Bongo Flava
Kazi yake Mtayarishaji
Ala Kinanda,Guitar, Kinakilishi
Miaka ya kazi mn. 1995 -
Studio Bongo Records
Ame/Wameshirikiana na Master Jay, Bonny Luv,Rajabu Marijani, Bizz Man, Boznia nk.

Paul Matthysse (maarufu kama P Funk, Halfani, Majani, Kinywele Kimoja, Mkono wa Mungu) ni mtayarishaji wa muziki na pia mmiliki wa Studio ya Bongo Records iliyopo jijini Dar es Salaam, Tanzania. Anaaminiwa na wengi kuwa ndiye mtayarishaji bora wa muda wote wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania.

P Funk ambaye ni nusu Mtanzania na nusu Mdachi, kama miaka ishirini iliyopita alikuwa na hisia za kupendelea muziki na pindi hadi kuamua kufanya kweli kuvutiwa kwake kupenda muziki ndio chanzo kikubwa kilichopelekea kufanikiwa katika muziki.

Kwenye miaka 1991-92 wakati bado yupo shule IST (International School Of Tanganyika). Alikuwa mtundu kwenye studio za pale shule kupigapiga midundo mbalimbali ya hapa na pale na kufoka-foka(Rap music) na pia alikuwa mbele sana kwa kupiga muziki kwenye pati mbalimbali na hapo alikuwa kupenda sana muziki kwa ujumla.

Elimu ya muziki na uzoefu wake

[hariri | hariri chanzo]

P-Funk alikwenda kimasomo ya Mlio (sound) engineering kwa miezi 18 pale Amsterdam, Netherland kabla ajaingia kwenye kutayarisha muziki. Alikuwa anajua kitu anachotaka kufanya. Mwaka 1995 akiwa na vifaa vyake vichache alianzisha kampuni yake ya kurekodi muziki nyumbani kwake. Na ni katika kipindi hicho hicho neno ’Bongo’lilipokuwa linatawala katika misemo ya kiswahili cha mitaani na lilikuwa linaelezea hali halisi ya maisha ya Dar es Salaam na ndio kipindi hicho album ya Bongo ilipozinduliwa.

Akiwa bado ni mtayarishaji muziki mdogo, amefanikiwa kupata umaarufu katika fani ya muziki na hasa katika milipuko ya nyimbo zenye ladha ya Bongo.

Anakubali kuwa amepata utaalam na mbinu kutokana na kuwafanyia kazi watayarishaji wengine wa muziki wa Kitanzania kama Master J, Bonny Love na Rico. Mawazo yake na namna ya kuyaoainisha na muziki ndio hasa ambacho kinafanya muziki wake ufanikiwe.

Wasanii aliowainua

[hariri | hariri chanzo]

Kwanza alianza kwa kumpandisha chati Juma Nature, ambaye ndio nyota wa nyimbo za Bongo Flava, akaendelea kwa kutayarisha santuri ya Solo Thang, AY, Zay B, Sista P, Mike T, Ze Pungu, Jay Mo, Chege, Temba, na baadhi ya wasanii wa TMK, pia alishawahi kufanya kazi na Professor Jay alipotoa santuri yake mwenyewe. Pia amefanya kazi ya kutoa midundo kwa msanii Afande Sele au Selemani Msindi wa Morogoro mfano Nyimbo ya Simba Dume aliyoshirikishwa Feruz. Amefanya kazi na wasanii wengi wa Bongo wakiwamo Wakongwe Mr.II (2 Proud) a.k.a. SUGU, Monduli Mobb, Gangwe Mobb, Hop Pot Family akiongozwa na Soggy Doggy, Manyema Family. Mwaka 2019, P funk Majani alimuibua Rapcha , msanii anayechipukia katika muziki wa Afrika Mashariki akiwa na uwezo wa ku-rap pamoja na kuimba: ndiye msanii pekee aliyepo chini ya nembo ya Pfunk Majani kwa sasa.

Tarehe 20 Desemba 2019 P funk Majani aliachia wimbo chini ya Bongo Records unaoitwa "Moto Unawaka" akimshirikisha Rapcha, TkiLLA na Msamiati.

Tuzo alizopata

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani wa Afrika bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu P. Funk kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.