Joseph Leonard Haule

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Professor Jay)
Professor Jay

Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Joseph Haule
Amezaliwa (1975-12-29)29 Desemba 1975
Asili yake Songea, Tanzania
Aina ya muziki Hip hop
Kazi yake Mbunge (jimbo la Mikumi - Mkoani Morogoro), Rapper, mtunzi wa nyimbo,
Miaka ya kazi 1989-hadi sasa
Ame/Wameshirikiana na Lady Jay Dee, Juma Nature, Inspector Haroun, Black Rhino, Simple X, Q Chillah, A.Y., Mangwair, Taff B.
Tovuti http://www.Professorjay.net

Joseph Leonard Haule (anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii Professor Jay ila zamani Nigga Jay; amezaliwa 29 Desemba 1975) ni Mtanzania msanii wa muziki wa hip hop na vilevile mwanasiasa wa Chama cha kisiasa cha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Amechaguliwa kuwa mbunge wa Mikumi kwa miaka 20152020. [1]

Nchini Tanzania anatazamika kama msanii aliyeweza kuwateka wazee wasikilize muziki wa Bongo Flava. Hasa kwa kibao alichofanya wakati yupo na kundi la Hard Blasters Crew - Chemsha Bongo. Kundi hilo ni moja ya makundi yaliyofanya muziki hup, ambao hujulikana kama 'muziki wa kizazi kipya', kukubaliwa na sehemu kubwa ya Watanzania.Jay vilevile ni moja kati ya waanzilishi au wasanii wa awali kabisa katika muziki wa hip hop ya Tanzania.

Maisha ya muziki[hariri | hariri chanzo]

Professor Jay alianza shughuli za muziki mnamo 1989 na alijiunga na kundi la 'Hard Blasters Crew' (HBC) mwaka 1994. Mwaka 1995 Jay na HBC walishinda kuwa kundi bora la Hip Hop nchini Tanzania.

Jay na HBC walitoa albamu ya kwanza iitwayo 'Funaga Kazi' mwaka 2000. Albamu hiyo inaaminika kwamba ilileta mapinduzi makubwa sana ya muziki wa Hip Hop nchini Tanzania. Albamu hii yenye ujumbe mzito ina nyimbo kama 'Chemsha Bongo' na 'Mamsapu' ambazo zilichangia kufanya muziki wa 'Bongo Flava' kuwa wa kila rika na kupewa heshima. Kabla ya hapo muziki huo ulionekana kuwa ni muziki wa wahuni.

Msanii binafsi[hariri | hariri chanzo]

Professor Jay aliamua kuwa msanii binafsi mnamo 2001 na muda mfupi baada ya hapo akatoa albamu yake ya kwanza iitwayo "Machozi Jasho na Damu". Albamu hii ilivuma haraka sana na kumfanya apate tuzo ya kuwa mtunzi bora wa Hip Hop nchini Tanzania kwa wimbo wake wa 'Ndio Mzee' kutoka kwenye albamu hiyo, wkifuatiwa na wimbo wa "Piga Makofi na Bongo Dar es Salaam"

Mwaka 2003 alitoa albamu ya pili iitwayo "Mapinduzi Halisi" ambayo nayo ilishinda tuzo ya Kili Music Awards kuwa albamu bora ya muziki wa Hip Hop nchini Tanzania kwa mwaka 2003. Albamu hii imebeba nyimbo kama "Zali la Mentali", "Msinitenge," na "Promota Anabeep"

Mwaka 2006 Januari alitoa albamu ya tatu iliyoitwa "J.O.S.E.P.H". Jina la albamu hii lilitokana na nyimbo iliyotoka Mwanzo kabla ya albamu kutoka. Wimbo huu ulichaguliwa kuwa wimbo bora wa Bongo Flava kwenye BBC na Radio One Awards.

Mpya imewahi kuteuliwa kuwa albamu bora ya Hip Hop, mtunzi bora wa nyimbo za Hip Hop, na Nyimbo bora ya Hip Hop ya mwaka kwenye Kili Music Awards. 2006."Nikusaidieje" na baadaye Kisima Music Awards ya Kenya ilikuwa Nyimbo bora ya Hip Hop na Video bora ya Hip Hop kutoka nchini Tanzania.

Tuzo Alizopata[hariri | hariri chanzo]

Albamu[hariri | hariri chanzo]

Hizi ni sehemu ya albamu za muziki alizotoa Nigga Jay

Alioshirikiana nao kimuziki[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Tovuti ya Bunge la Tanzania, iliangaliwa Mei 2017

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Joseph Leonard Haule kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.