Inspector Haroun

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Inspector Haroun (Kushoto) na Lady Jay Dee

Haroun Rashidi Kahena (maarufu kama Inspector Haroun) ni mwanamuziki kutoka Temeke, Dar es Salaam, nchini Tanzania.

Yuko katika kundi la Tmk Wanaume Halisi. Inspector Haroun ni mtoto wa mzee Kahena aishiye huko Temeke Mikoroshini, jijini Dar es Salaam.

Maisha ya muziki[hariri | hariri chanzo]

Haroun alianza kazi muziki mnamo miaka ya 1990 na amefanya kazi kadhaa kipindi cha nyuma na wanamuziki wengine tofauti kabla ya kujiunga na Tmk Wanaume Halisi. Alitoa nyimbo ya kwanza mwaka 1998, 'Mauzauza', akiwa na Luteni Karama kwenye kundi la Gangwe Mobb. Baada ya hapo wakatoa nyingine mwaka 2000 'Mtu Be,' kisha wakatoa Wimbo wa 'Mtoto wa Geti Kali' ulimpatia umaarufu mkubwa. Aliutoa wimbo huu peke yake ingawa alikuwa bado yupo katika kundi la Gangwe Mobb.

Albamu alizotoa akiwa Gangwe Mobb[hariri | hariri chanzo]

  • Simulizi La Ufasaha @(2001)
  • Nje Ndani @(2002)

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Inspector Haroun kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.