Lady Jay Dee
Lady Jay Dee | |
---|---|
Jide akiwa katika pozi
| |
Maelezo ya awali | |
Jina la kuzaliwa | Judith Daines Wambura Mbibo |
Pia anajulikana kama | Binti Machozi Komandoo Jidee Jay Dee |
Amezaliwa | 6 Juni 1979 |
Asili yake | Mkurya |
Aina ya muziki | R&B Bongo Flava Afro-Pop |
Kazi yake | Mwanamuziki |
Ala | Sauti |
Miaka ya kazi | 1999-hadi leo |
Studio | MJ Records FM Studio Bakunde Production |
Ame/Wameshirikiana na | Mr. II Professor Jay Juma Nature Inspector Haroun Q. Chillah Mwana FA |
Judith Daines Wambura Mbibo (anafahamika zaidi kwa jina la kisanii kama Lady Jay Dee; amezaliwa mkoani Shinyanga 15 Juni 1979) ni mwanamuziki wa Bongo Flava-Afro pop kutoka nchini Tanzania[1].
Maisha ya awali
Judith Wambura alizaliwa na Martha na Lameck Isambua Mbibo ambao ndio wazazi wake. Alianza kuimba akiwa na umri wa miaka saba. Alianzia kuimba kanisani kama ilivyo kwa wasanii wengi. Baada ya kumaliza shule, Lady Jaydee aliwahi kufanya kazi Clouds FM kabla ya kuamua kujiingiza kwenye masuala ya muziki hapo mnamo miaka ya 2000.[2]
Shughuli za muziki
Alianza kujibebea heshima katika medani ya muziki kunako mwaka wa 2000 baada ya kutoa albamu yake ya kwanza iliyokwenda kwa jina la "Machozi" na kutoa single kadhaa kutoka katika albamu hiyo na kumfanya kuwa mwanamama wa kwanza katika bongo flava kwa kutumia gharama kubwa ya ujenzi wa albamu katika historia ya muziki wa kizazi kipya.
Lady Jay Dee ni msanii mwenye kumiliki studio yake mwenyewe ya kurekodia. Studio inakwenda kwa jina la Jag Records.
Jay Dee, alishawahi kuchaguliwa kuwa Mwanamuziki Bora wa Kike wa Tanzania kwa muziki wa R&B mnamo 2002, na kutumbuiza katika Kora All Africa Designers Competition, na kutuzwa "Albamu Bora ya R&B" katika Tuzo za Muziki Tanzania kunako tar. 6 Agosti 2004. Kunako mwezi wa Julai 2005, ameshinda tuzo ya "video bora ya msanii wa kike kwa Afrika Kusini".
Muziki
Albamu zake
Jay Dee, ametoa albamu saba za muziki[3]:
- Machozi (2000)
- Binti (2003)
- Moto (2005)
- Shukrani (2007)
- Ya 5. The Best of Lady Jaydee (2012)
- Nothing But The Truth (2013)
- Woman (2017)
Marejeo
- ↑ https://www.jamiiforums.com/threads/historia-ya-lady-jaydee.522321/
- ↑ "Manka kwenye BC". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-11-05. Iliwekwa mnamo 2009-10-13.
- ↑ https://en.wikipedia.org/wiki/Lady_Jaydee
Viungo vya Nje
- JD kwenye Facebook
- Swahili Remix Archived 24 Januari 2007 at the Wayback Machine.
- Bongo Flava Archived 8 Desemba 2006 at the Wayback Machine.
- Brief biography
- [1]
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani wa Afrika bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Lady Jay Dee kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |