Mwana FA

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mwana Fa
Jina la kuzaliwa Hamis Mohammed Mwinjuma
Amezaliwa Tanga
Asili yake Muheza, Tanzania
Aina ya muziki Hip hop
Kazi yake Mwanasiasa
Rapper, mtunzi wa nyimbo,
Ame/Wameshirikiana na Lady Jay Dee, Vanessa Mdee, Inspector Haroun, A.Y. (mwanamuziki), Mangwair


Hamis Mohammed Mwinjuma, anayejulikana pia kama Mwana FA[1] ni mwanamuziki, mjumbe wa bodi ya Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), na mwanasiasa[2] anayehudumu kama Mbunge wa jimbo la Muheza tangu Novemba 2020. Anajulikana kwa nyimbo zake kama Endelea Tu na Unanijua Unainiskia[3].

Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Hamis Mwinjuma alizaliwa Muheza, Tanga, Tanzania. Mwaka 2016 alifunga ndoa na Bi Helga Mwinjuma wakifanikiwa kupata wana watoto wawili. Mwinjuma na familia yake wanaishi jijini Dar es Salaam, Tanzania[4].

Elimu[hariri | hariri chanzo]

MwanaFa alianza elimu yake ya msingi katika shule ya msingi ya Mdote huko Muheza[5]. Alijiunga na chuo cha Dar es salaam Institute of Technology kwa ajili ya masomo yangazi ya juu. Hata hivyo alikatiza masomo yake miezi minne tu baada ya udahili ili kujiunga na elimu ya upili katika shule ya sekondari ya Ununio Islamic akienda na mchepuo wa fizikia, kemia na hisabati[6]. Alifanya Stashahada ya Juu ya uchumi kwa mwaka mmoja katika Taasisi ya Fedha.  Baadaye alifanikiwa kufanya Shahada ya Uzamili ya Sayansi ya Fedha kutoka katika taasisi hiyo hiyo.  Mwinjuma alihitimu taaluma ya Usimamizi wa uchumi mwaka 2007, pia ana cheti cha teknolojia ya habari na Shahada ya Uzamili ya Fedha kutoka Coventry, Uingereza.

Shughuli za Muziki[hariri | hariri chanzo]

Mapenzi yake na muziki yalianza kuonekana tangu akiwa na umri mdogo wa miaka kumi na miwili.  Alianza kuimba akiwa shule ya msingi.  MwanaFa aliunda kundi lake la kwanza, lililoitwa Black Skin hiyo ilikua mwaka 1995 ambalo lilikuwa na wanafunzi wenzake Robby Ras na Generics.  Kundi hilo liliibuka katika nafasi ya tatu kwenye mashindano ya Hip Hop ya Tanga mwaka mmoja baadaye.  Kwa bahati mbaya kundi hilo halikudumu kwa muda mrefu kwani wanachama walikuwa na njia tofauti katika maendeleo kitaaluma.  Hata hivyo, Mwinjuma aliendelea kunoa kipaji chake akiwa katika shule ya upili na kuanza kutoa vibao bora zaidi happ baadaye[7].

Shughuli za siasa[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 2020, Mwinjuma alijiunga na ulingo wa siasa nchini Tanzania alipowania kiti cha ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi.  Akishinda dhidi ya Yosepher Komba wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa kupata kura 47,578 za ubunge wa Jimbo la Muheza[8].

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Mwana FA and Babu Tale cleared to vie for parliamentary seats (en). The Citizen (2020-10-29). Jalada kutoka ya awali juu ya 2022-10-17. Iliwekwa mnamo 2022-10-17.
  2. Tanzania: Umuhanzi Mwana FA yinjiye mu nteko, Professor Jay arasohoka (rw). BBC News Gahuza (2020-10-30). Iliwekwa mnamo 2022-10-17.
  3. Mwana FA aeleza kilichotokea ajali aliyopata | East Africa Television (en). eatv.tv (2021-08-31). Iliwekwa mnamo 2022-10-17.
  4. Barbara Davis (2021-07-29). MwanaFa biography: wife, family, politics, songs, life story (en). Tuko.co.ke - Kenya news.. Iliwekwa mnamo 2022-10-17.
  5. Tanzanian Rapper Mwana FA Tests Positive for Coronavirus (en). okayafricasite. Iliwekwa mnamo 2022-10-17.
  6. Solomon Mwesigwa (2020-11-12). Tanzanian Bongo rapper Mwana FA sworn in as Muheza MP (en-US). MBU. Iliwekwa mnamo 2022-10-17.
  7. Mpoki Thomson (2020-12-09). Kenya: Mwana FA, AY to Return Sh100 Million Awarded in Copyright Case (en). allAfrica.com. Iliwekwa mnamo 2022-10-17.
  8. Dereva aliyehusika na ajali ya Mwana-FA atibiwa chini ya ulinzi (en). Mwananchi (2021-08-31). Iliwekwa mnamo 2022-10-17.