Nenda kwa yaliyomo

Vanessa Mdee

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Vanessa Mdee

Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Vanessa Hau Mdee
Pia anajulikana kama Vee Money
Amezaliwa (1988-06-07)7 Juni 1988
Asili yake Arusha, Tanzania
Aina ya muziki
Kazi yake
Miaka ya kazi 2007 - hadi sasa
Tovuti http://www.vanessamdee.com

Vanessa Hau Mdee (amezaliwa jijini Arusha tarehe 7 Juni 1988) ni mwanamuziki wa Tanzania, rapa, mtunzi wa nyimbo na mtangazaji wa televisheni na redio. Jina lingine la Vanessa Mdee ni Vee Money. Vanessa Mdee anafahamika kwa kuwa mtanzania wa kwanza kuwa mtangazaji wa MTV.[1] Vanessa alikuwa mtangazaji wa Epic Bongo Star Search na Dume Challenge ndani ya ITV Tanzania. Mwishoni mwa mwaka 2012, Vanessa alijiunga na B'Hits Music Group.[2]

Baada ya kujiunga na B'hits Music Group, Mdee alishirikiana na rapa kutoka Tanzania A.Y. kwenye wimbo wa Money. Pia, alishirikiana na Ommy Dimpoz, msanii wa Bongo Flava, kwenye wimbo wa Me and You, ambao baadaye ulichaguliwa kuwa wimbo bora wa mwaka kwenye Tuzo za Muziki za Kilimanjaro za mwaka 2013[3]. Mnamo 2015 na 2016, alitoa nyimbo tatu ("Nobody But Me", "Never Ever" na "Niroge") ambazo zilipokelewa vyema. Mwaka 2018, alisainiwa chini ya lebo na Universal Music Group.[4]

Maisha yake ya awali na elimu yake

[hariri | hariri chanzo]

Vanessa Mdee amekuwa akifahamu tamaduni mbalimbali baada ya kuishi katika miji mbalimbali duniani kama vile New York, Paris, Nairobi na Arusha.

Alipata elimu ya sekondari katika shule iitwayo Arusha Modern High School. Alipata elimu ya juu katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Afrika Mashariki (Kiingereza: Catholic University of Eastern Africa) na kuchukua shahada ya Sheria. Alianza kujishughulisha na ubunifu na sanaa.

Kazi yake

[hariri | hariri chanzo]

2007: Utafutaji wa mtangazaji wa MTV

[hariri | hariri chanzo]

Mwanzoni mwa mwaka 2007, Mdee alipata fursa ya kushiriki katika Utafutaji wa mtangazaji wa MTV (Kiingereza: MTV VJ Search) huko Dar es Salaam. Baadaye, alijiunga na Carol na Kule kuandaa Coca Cola Chart Express. Mnamo mwaka 2008, Vanessa Mdee alikuwa anaishi nchini Tanzania na nchi nyingine za Afrika huku akijihusisha na utayarishaji wa matukio huko Nigeria, Afrika Kusini, Kenya, Msumbiji, Angola, Uganda, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Pia alijulikana nchini Marekani na Brazil.

2008: Shirika la Staying Alive

[hariri | hariri chanzo]

Mnamo mwaka 2008, Vanessa Mdee alifanya kazi na Shirika la Staying Alive (Kiingereza: Staying Alive Foundation). Alitembelea Uwanja wa Fisi na Balozi maalum wa Shirika la Staying Alive, Kelly Rowland. Pia alijiunga na kampeni ya Zinduka iitwayo Malaria No More, kampeni hii inalenga kukomesha malaria.

East Africa's Got Talent

[hariri | hariri chanzo]

Mnamo Julai 2019, Vanessa Mdee alitambulishwa kama mmoja wa majaji wanne waanzilishi wa msimu wa kwanza wa East Africa's Got Talent, ambayo ilianza kuonyeshwa Agosti 2019.[5]

Money Mondays

[hariri | hariri chanzo]

Vanessa Mdee alitoa albamu yake ya kwanza 'Money Mondays' tarehe 15 Januari 2018. Albamu hii ina jumla ya nyimbo kumi na nane, huku mbili zikiwa kama nyimbo za ziada na kumi na sita kama nyimbo rasmi.[6] Baadhi ya nyimbo ni pamoja na Bambino amemshiikisha Reekado Banks, Cash Madame, Bounce na Kisela amemshirikisha Mr.P wa P Square.

MTV Shuga

[hariri | hariri chanzo]

Vanessa Mdee alionekana kwenye mfululizo wa tamthilia ya televisheni ya MTV Shuga Down South kama Stormi the glam madam.[7]

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-04-11. Iliwekwa mnamo 2020-04-11.
  2. https://www.bbc.co.uk/music/artists/89a576d7-45b0-4e6d-9035-20107206f035
  3. "Tanzania Music Awards", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2022-05-12, iliwekwa mnamo 2022-06-02
  4. "Vanessa Mdee: "It's Tough to Be a Female Artist, You Have to Work Five Times Harder Than the Men"". OkayAfrica (kwa Kiingereza). 2019-02-11. Iliwekwa mnamo 2022-06-02.
  5. "Singer Vanessa Mdee named as judge at East Africa Got Talent 2019". The Citizen (kwa Kiingereza). 2021-04-10. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-06-02. Iliwekwa mnamo 2022-06-02.
  6. "Kenya breaking news | Kenya news today | Capitalfm.co.ke » Capital News". Capital News (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2022-06-02.
  7. Esther Muchene. "Vanessa Mdee makes MTV Shuga acting debut". Standard Entertainment and Lifestyle (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-06-02.
Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Vanessa Mdee kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.