Bounce

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
“Bounce”
“Bounce” cover
Kava ya Bounce
Single ya Vanessa Mdee akiwa na Maua Sama na Tommy Flavour
kutoka katika albamu ya Money Mondays
Imetolewa 14 Novemba, 2017
Muundo Upakuzi wa mtandaoni
Imerekodiwa 2017
Aina Bongo Flava, pop, afro-pop
Urefu 3:41
Studio BKej Studios
Mtunzi Vanessa Mdee
Maua Sama
Tommy Flavour
Mtayarishaji Breezy
Mwenendo wa single za Vanessa Mdee akiwa na Maua Sama na Tommy Flavour
"Kisela"
"(2017)"
"Bounce"
"(2017)"
"Wet"
(2018)

"Bounce" ni jina la wimbo uliotoka tarehe 14 Novemba, 2017 kutoka kwa msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Tanzania - Vanessa Mdee akimshirikisha Maua Sama na Tommy Flavour.[1] Wimbo unatoka katika albamu ya Money Mondays na wa tatu kutolewa kama singo kutoka katika albamu hiyo. Wimbo umetayarishwa na Breezy kupitia studio za BKej Studios za nchini Tanzania. Wimbo umechukua sampuli ya wimbo wa "Bounce Along" ulioimbwa na "Wayne Wonder" na kutia ladha za Kiafrika zaidi. Ndani yake wanafuata mtindo kama ule wa Monique na Brandy Norwood katika "The Boy Is Mine".[2] Wanatambiana kama kwa maneno ya kuonesheana ujuzi zaidi katika mapenzi kwa mpenzi wao. Nessa anatamba kwa kusema "yeye pekee ndiye anayeweza kumfikisha" kwa maneno ya Kiingereza "Only me can turn him on". Huku Maua nae akijibu kwa kusema:

"Husinifanye me, ni poyoyo,
Lengo lako girl,
Niachane naye nenda zako hukoo,
I want you to know, usije ukaniliza girl."

Wimbo mzima ni wa majibizano kati ya watoto wa kike wawili dhidi ya bwana mmoja.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]