ITV Tanzania

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


ITV Tanzania
Nembo ya ITV Tanzania
Nembo ya ITV Tanzania
Kutoka mji Dar es salaam
Nchi Tanzania
Eneo la utangazaji Kote duniani
Kituo kilianzishwa mwaka 1994
Mwenye kituo IPP Limited
Programu zinazotolewa Redio na runinga
Tovuti itv.co.tz

ITV Tanzania - Independent Television Limited (ITV) ni kampuni ya utangazaji nchini Tanzania inayomilikiwa na kampuni ya IPP Media[1].

ITV ilikuwa chaneli ya kwanza ya televisheni kuanzishwa Tanzania Bara. Ilianza shughuli zake mwaka 1994 ikiwa na kituo kimoja cha televisheni na kituo kimoja cha redio ambavyo ni ITV - Tanzania na Radio One.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Tarehe 10 Juni 1994, Independent Television (ITV) ilianza kurusha matangazo yake ya televisheni, ilikuwa chaneli ya televisheni ya kisasa zaidi nchini na ilianzishwa na Reginald Mengi.

ITV ilirusha matangazo yake kuanzia saa sita za usiku hadi saa sita za mchana. Wakati wa matukio maalum, kama vile Olimpiki ya Majira ya joto ya 1996 huko Atlanta, ITV iliongeza muda wake wa kurusha matangazo. Kwa sababu ya transmita zake mbili za kW zilizowekwa kwenye eneo la juu zaidi jijini Dar es Salaam, Mikongo, matangazo yake yalifika ndani ya eneo la kilomita 45, na kwa kuwa bahari inakuza mawimbi, matangazo yaliweza kufika Zanzibar.[2]

Tarehe 2 Novemba 1995, Rais wa wakati huo Ali Hassan Mwinyi alizindua kituo cha kidijitali cha ITV chenye  mfumo wa uplink maeneo ya Mikocheni, kilianzishwa ili kusambaza programu za ITV na Radio One kwa maeneo yote ya Tanzania. Matangazo yalipitishwa kidijitali kupitia satelaiti ya mawasiliano ya INTELSAT 601 hadi kwenye kituo cha mtandao wa ORBICOM jijini Johannesburg. Kutoka hapo mawimbi yaliunganishwa kwa transiponda ya PAS-4 ambayo ni mali ya PanAmSat na kisha kuunganishwa kidijitali na mikoa iliyochaguliwa nchini Tanzania. Awamu ya kwanza ya upanuzi wa ITV ilianza tarehe 2 Novemba kwa kurusha programu za kituo hicho kwa televisheni 18 za jumuiya kote nchini, maeneo hayo ya kijamii yalianzishwa Arusha, Bukoba, Dodoma, Iringa, Kigoma, Lindi, Mbeya, Morogoro, Moshi, Mtwara, Musoma, Mwanza, Shinyanga, Singida, Songea, Sumbawanga, Tabora, na Tanga. Hadi watu 5,000 walitazama vipindi vya ITV kwenye skrini kubwa zilizowekwa katika maeneo hayo.

Mnamo mwaka 2009 kampuni ilizindua Capital Television na Capital Radio.

Mwaka 2013, ITV ilitunukiwa tuzo ya Superbrand namba moja nchini Tanzania [3] na kutambulika kuwa miongoni mwa chapa 100 zilizoongoza Afrika ya Mashariki kwa mwaka 2015 hadi 2017. Mnamo mwaka wa 2014, ITV ilitunukiwa tuzo ya Most Compliant Tax Payer na ilikuwa taasisi pekee ya utangazaji kupokea tuzo kama hiyo.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. admin (2017-04-28). "About us". ITV - Independent Television (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-06-02. 
  2. Sturmer, Martin (1998). The Media History of Tanzania. Ndanda Mission Press, 1998. ku. 82 – 83. ISBN 9789976635928.  Check date values in: |accessdate= (help);
  3. admin (2017-04-28). "Superbrand". ITV - Independent Television (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-06-02. 

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]