MTV

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Hii ni lebo ya MTV

MTV ni chaneli ya muziki iliyopo jijini New York, Marekani. Ilizinduliwa mnamo Agosti 1, 1981) na hutumika kama mali kuu ya MTV Entertainment Group, sehemu ya Paramount Media Networks ikiwa ni mgawanyiko wa Paramount Global.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Mawazo ya televisheni ya muziki yalianza katika miaka ya 1960. Bendi ya muziki ya The Beatles walitumia video za muziki kutangaza rekodi zao kuanzia katikati ya miaka ya 1960. Filamu yao iliyotoka mwaka 1964 ya A Hard Day's Night, na uimbaji wa wimbo "Can't Buy Me Love", zilifanya MTV kumtunukia tuzo ya (kuvumbua video ya muziki) mkurugenzi wa filamu hiyo Richard Lester.[1]

Mnamo 1967, kampuni iliyopo Los Angeles iitwayo Charlatan Productions ilianza kutoa filamu za matangazo kwa vikundi vya rock kwa mbinu ya kipekee, iliyohusisha kutafsiri nyimbo binafsi kwa kutengeneza maandishi asilia na matukio ya kisanii ili kuendana. Charlatan ilianzishwa na watengenezaji filamu Peter Gardiner na Allen Daviau; wote wawili walikuwa watayarishaji wa matukio maalamu kwenye filamu miaka hiyo.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Richard Lester: A hard day's life (en). Salon. Jalada kutoka ya awali juu ya 2012-11-26. Iliwekwa mnamo 2012-11-26.