Nenda kwa yaliyomo

Ommy Dimpoz

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ommy Dimpoz
Taarifa za awali
Jina la kuzaliwaOmary Faraji Nyembo
Amezaliwa12 Septemba 1987 (1987-09-12) (umri 36)[1]
Dar es Salaam, Tanzania
Kazi yakeMwimbaji na Mfanyabiashara
AlaSauti
Ameshirikiana naAli Kiba, Diamond Platnumz, Dully Sykes

Omary Faraji Nyembo (amezaliwa 12 Septemba, 1987) ni mwimbaji wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Tanzania ambaye anajulikana kwa jina la kisanii kama Ommy Dimpoz. Ommy alianza kuvuma kwa wimbo wake wa Nai Nai aliomshirikisha Ali Kiba, Baadaye, Mama alioshirikishwa na Christian Bella, Me and You alioshirikishwa na Vanessa Mdee, Utamu alioshirikishwa na Dully Sykes, Hello Baby alioshirikishwa na Avril kutoka Kenya, Cheche, Achia Body, Tupogo, Ndagushima, Wanjera na Kajiandae. Ommy Dimpoz ni msanii mwenye masihara na maneno mengi ya kuchekesha. Sawa na Rayvanny wa WCB. Ommy ni moja kati ya wasanii ambao wanajali sana faragha za maisha yao.

Awali mwaka 2016 kulikuwa na gumzo kubwa baada ya Nay wa Mitego kumwimba vibaya Ommy kwenye wimbo wake na kumshutumu kama shoga. Baadaye Ommy akajibu kwa kuonesha picha ya demu wake na ikaja kugundulika kuwa Nay wa Mitego ana kibamia.[2] Ommy ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Pozi kwa Pozi Entertainment ambayo meneja wake (Mubenga) aliachia ngazi mwaka wa 2016.[3] Tangu wimbo wa Cheche (2017), amekuwa chini ya lebo ya Rockstar4000 ambayo iko chini ya Ali Kiba.[4][5]

Mwaka wa 2018, ulikuwa mgumu sana kwa Ommy Dimpoz. Afya yake ilitetereka sana baada ya kufanyiwa vipimo Tanzania na kuonekana ana kansa. Lakini baada ya kwenda Kenya kwa moja ya marafiki zake wanaofanya kazi pamoja katika muziki ili kufanyiwa uchunguzi zaidi, napo daktari wa huko alipendekeza apelekwe Afrika Kusini kwa uchunguzi zaidi. Akiwa Afrika Kusini aligundulika kama ana tatizo katika njia kuu ya kupitishia chakula. Daktari wa Afrika Kusini walitengeneza njia mpya ya kupitishia chakula badala ya ile njia ya asili. Ili kufanikisha hili, ilibidi utumbo uvutwe juu. Hivyo kina cha tumbo kimepungua kutoka hali ya umbo halisi. Hata uwezo wa kula umepungua, akila anashiba mapema sana tofauti na watu ambao hawajafanyiwa upasuaji huu. Kabla ya upasuaji, Ommy alilamikia sana kukosa pumzi, sauti kuwa chini na kadhalika. Hali halisi alifanyiwa upasuaji wa koromeo. Hali ambayo ilisababishwa na sumu iliyowekwa kwenye chakula. Ommy hajui ni wapi alifanyiwa hivyo.[6] [7][8][9]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Ommy Dimpoz Biography, Age, Girlfriend, House, Real Name & Instagram - Kizimedia blogu
  2. Ommy Dimpoz Amuonyesha Mpenzi wake Hadharani na Kumchana Nay wa Mitego Baada ya Nay Kumuhusisha na Ushoga Kwenye Nyimbo yake Udaku Special blogu, 2016.
  3. Mubenga awatema Ommy Dimpoz na Nedy Music EATV - 2016
  4. Ommy Dimpoz ajiunga na Alikiba kwenye label mpya Archived 7 Septemba 2019 at the Wayback Machine. Ghafla wavuti, 2017.
  5. Ali Kiba amsainisha Ommy Dimpoz RockStar4000 wavuti ya Dar24, 2017
  6. "Fahamu ugonjwa unaomsumbua Ommy Dimpoz, mtaalamu wa afya aeleza vyanzo vyake na kutoa tahadhari kwa wasanii (+Audio)". Bongo5.com (kwa American English). 2018-07-20. Iliwekwa mnamo 2018-12-26.
  7. Diana Benjamin (2018-08-27). "Ommy Dimpoz Afunguka Kuhusu Afya Yake Kwa Sasa". Ghafla! Tanzania (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-10-28. Iliwekwa mnamo 2018-12-26.
  8. "Daktari azungumzia ugonjwa unaomsumbua Ommy Dimpoz". Mwananchi (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2018-12-26.
  9. IMEWEKWA NA George Mganga. "OMMY DIMPOZ AFUNGUKA KUHUSIANA NA MAENDELEO YA AFYA YAKE HUKO AFRIKA KUSINI". Iliwekwa mnamo 2018-12-26.
Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ommy Dimpoz kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.