Nenda kwa yaliyomo

Dully Sykes

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Abdul Sykes (alizaliwa 4 Desemba, 1980),[1] ni mwanamuziki wa Tanzania. Anakadiriwa kuwa mmoja wa waanzilishi wa mwanzo wa muziki wa kizazi kipya Tanzania maarufu kama Bongo Flava.

Dully Sykes
Jina la kuzaliwa Abdul Sykes
Pia anajulikana kama Mr. Misifa
Amezaliwa 4 Desemba 1980 (1980-12-04) (umri 44)
Asili yake Tanzania
Aina ya muziki Hip hop
R&B
bongo Flava
Pop
Kazi yake Mwimbaji
Mtayarishaji wa muziki

Dully Sykes kama anavyojulikana kwa majina, Mr. Chicks au Mr. Misifa Ni mjukuu wa Abdulwahid Sykes, mwanaharakati wa kudai uhuru wa Tanganyika. Sykes anajulikana kwa nyimbo zake maarufu zinatokana na matukio ya kweli kama Historia ya Kweli, Julieta, Leah, na Salome. Kufuatia kutolewa kwa albamu yake ya kwanza, Historia ya kweli, mwaka wa 2003.Sykes ameendelea kubaki katika chati za juu za muziki wa Tanzania akishirikiana na wasanii wakubwa wa muziki kutokea nchini Tanzania kama Harmonize na Marioo

Kili Music Awards

[hariri | hariri chanzo]

Hizi ni tuzo alizoshiriki au kupokea kutoka Kili Music Awards katika misimu tofauti[2].

MwakaMteule / kaziTuzoMatokeo
2012[3]Bongo FlavaAlichaguliwa
2012Bongo FlavaWimbo bora wa AfropopAlichaguliwa
2012Msanii bora wa kiumeAlichaguliwa
2010ShikideWimbo bora wa Dancehall/RaggaAlichaguliwa
2008Baby CandyWimbo bora wa Reggae/RaggaAlichaguliwa
2007[4]Dhahabu akiwa na Mr. Blue na JoslinWimbo bora wa ushirikianoAlichaguliwa
2004HandsomeAlbamu boraAlichaguliwa
2012Maneno Maneno akiwa na Queen DarleenWimbo bora wa Dancehall/RaggaAlishinda
2011Action akiwa na Ms. Triniti, CPWAA na NgwairVideo BoraAlishinda
2011ActionWimbo bora wa Dancehall/RaggaAlishinda
  1. Madenge (2021-08-18). "Quick Snapshot: Tanzanian Musician Dully Sykes". UnitedRepublicofTanzania.com (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2022-10-17.
  2. "Kilitime". web.archive.org. 2004-12-04. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2004-12-04. Iliwekwa mnamo 2022-10-17.
  3. "Kili awards 2012 Nominees hawa hapa! – Bongo5.com". bongo5.com. Iliwekwa mnamo 2022-10-17.
  4. "Kilitime". web.archive.org. 2011-07-13. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-07-13. Iliwekwa mnamo 2022-10-17.
Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Dully Sykes kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.