Harmonize

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Harmonize
Jina la kuzaliwa Rajab Abdul Kahali
Pia anajulikana kama Harmonize
Amezaliwa 15 Aprili 1994 (1994-04-15) (umri 25)
Asili yake Mtwara,Tanzania
Aina ya muziki Bongo Flava,Afro Pop
Kazi yake Mwimbaji-mtunzi, mtayarishaji wa rekodi
Ala Piano, sauti
Miaka ya kazi 2011–mpaka sasa
Studio Wasafi Records
Ame/Wameshirikiana na Rayvanny, Diamond Platnumz
Tovuti Tovuti Halisi

Harmonize (kwa jina lake halisi Rajab Abdul Kahali; mara kadhaa hujiita "Konde Boy"; amezaliwa Chitoholi, mkoa wa Mtwara, 15 Aprili 1994) ni mwimbaji na mtunzi wa muziki kutoka Tanzania.

Harmonize ana asili ya Mtwara. Alianza kuvuma kwa kibao chake cha kwanza cha "Aiyola" (2015), Bado (2016), Matatizo (2016) na baadaye akatoa nyimbo na msanii mwenzie kutoka lebo moja ya wcb ambaye ni Diamond Platnumz.

Kwa ngwaru ni wimbo ambao ulibamba karibia maeneo yote ya Afrika ya Mashariki akatoa kibao kingine kiitwacho inama nyimbo ambayo aliimba na msanii kutoka nje ya tanzania ambaye anaitwa burna na dimond platnimz alikuwepo kwenye huo wimbo na sasa hivi anatamba na kibao kiitwacho never give up wimbo ambao unaelezea historia ya maisha yake kuanzia alivyo kuwa na maisha magumu sana. Harmonize anasimamiwa na Joel Joseph au kwa jina lingine Mr Puaz.

Maisha ya Awali[hariri | hariri chanzo]

Harmonize alisoma katika shule ya sekondari Mkundi iliyopo huko mjini Mtwara. Baada ya kumaliza elimu yake ya sekondari, Harmonize alielekea jijini Dar es Salaam ambako alijipatia riziki yake ya kila siku.

Harmonize mwanzoni alibeba maji ili kupata tonge la chakula, pia alikua akiuza kahawa kwa wafanya biashara wengine na wakazi wa Kariakoo huko jijini Dar es Salaam kabla ya sauti yake kutambulika mitaani kisha baadae kuchukuliwa na lebo ya Diamond platnumz ijulikanayo kama WCB (Wasafi classic baby). Kwa sasa ameamua kujiondoa katika lebo hiyo kutokana na sababu ambazo hazikuwekwa wazi.

Alianza kujihusisha na muziki mnamo mwaka 2011 ambapo alitoa nyimbo mbalimbali lakini hazikuweza kupata umaarufu mkubwa mpaka pale ambapo alikutana na Diamond Platinumz mnamo mwaka 2015 na kuanza kufanya mziki pamoja naye.

Diskografia[hariri | hariri chanzo]

Nambari Mada ya wimbo Mwaka
1. Aiyola 2015[1]
2. Bado ft Diamond Platnumz 2016
3. Matatizo 2017
4. Happy Birthday 2017
5. Shula 2017
6. Sina 2017
7. Niambie 2017
8. Dont go 2017
9. Nishachoka 2017
10. Nakupenda 2017
11. Kwa ngwaru ft. Diamond platnumz 2018
12. Dm chick 2018
13. Atarudi 2018
14. Paranawe ft. Rayvanny 2018
15. Niteke 2019
16. Show me what you gat ft. Yemi Alade 2019
17. Kainama ft. Diamond Platnumz na Burna boy 2019
18. Ndoenda 2019
19. Never give up 2019

Tuzo na teuzi[hariri | hariri chanzo]

Mwaka Kazi iliyoteuliwa Tuzo Matokeo
2016 Bado Ft Diamond Platnumz WatsUp TV Tuzo la Video Bora zaidi ya Mwimbaji Chipukizi Ameshinda[2]
Yeye Mwenyewe African Muzik Magazine Awards (AFRIMMA) kwa Mwimbaji Chipukizi Ameshinda[3]
African Entertainment Awards (AEAUSA) kwa Msanii Chipukizi Bora zaidi Ameshinda[4]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Musical notes.svg Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Harmonize kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.