Queen Darleen
Queen Darleen | |
---|---|
Queen Darleen akiwa ameshika tuzo ya "Kili" baada ya kuibuka mshindi wa tuzo hizo kwa wimbo bora mwaka 2012.
| |
Maelezo ya awali | |
Jina la kuzaliwa | Mwanahawa Abdul Juma |
Amezaliwa | 4 Novemba 1985 |
Asili yake | Kigoma,Tanzania |
Aina ya muziki | Bongo Flava,Afro Pop |
Kazi yake | Mwimbaji-mtunzi |
Ala | sauti |
Miaka ya kazi | 2001–mpaka sasa |
Studio | Wasafi Records |
Ame/Wameshirikiana na | Dully Sykes, Inspector Haroun, Ali Kiba, Shilole, Rayvanny, Diamond Platnumz, Harmonize, Lavalava (mwanamuziki), Mbosso, Rich Mavoko |
Mwanahawa Abdul Juma (amezaliwa 4 Novemba 1985) ni msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Tanzania.
Queen alianza muziki mwanzoni mwa miaka ya 2000 akiwa ameshirikishwa na Dully Sykes katika wimbo wake wa Historia ya Kweli au maarufu Sharifa na Mtoto wa Geti Kali wa Inspector Haroun kabla kwenda kufanya muziki wa kujitegemea na 2006 kutoka kibao cha "Wajua Nakupenda alichofanya na Ali Kiba chini ya utayarishaji wake KGT na usimamizi wa DJ Guru Ramadhani. Mwaka wa 2012 alishinda tuzo ya Kili kwa wimbo bora wa Ragga/Dancehall.[1]
Baada ya harakati za muda mrefu, hatimaye amesainiwa na lebo ya WCB Wasafi iliyo chini ya Diamond Platnumz ambaye ni ndugu yake wa damu kwa upande wa baba.[2] Akiwa na WCB ametoa wimbo wake wa kwanza Kijuso uliotoka rasmi tarehe 17 Februari 2017 aliofanya na Rayvanny.[3] Halafu Ntakufilisi (Novemba 9 2017[4]), na Touch (22 Novemba 2017[5]). Vilevile alishiriki kuimba katika wimbo wa pamoja wa WCB Zilipendwa ulitoka tarehe 25 Agosti 2017.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ QUEEN DARLEEN:DADA WA DIAMOND ALIYETIWA NDIMU NA TUZO YA KILI Archived 21 Januari 2018 at the Wayback Machine. ingizo la 20 Aprili, 2012 - katika blogu ya Sports Lady.
- ↑ Je! Unafahamu? Diamond na Queen Darlin wanachangia Baba! katika wavuti ya Bongo5. Ingizo la June 8, 2012.
- ↑ RAYVANNY - QUEEN DARLEEN FT RAYVANNY - KIJUSO (OFFICIAL VIDEO) ingizo la Feb 17, 17.
- ↑ Queen Darleen - Ntakufilisi (Official Video) ingizo la Nov 9, 17.
- ↑ Queen Darleen -Touch (Official Video)
Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Queen Darleen kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |