Rich Mavoko

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Richard Martin Lusinga (Amezaliwa mnamo 26 Oktoba 1990), maarufu anayejulikana kama Rich Mavoko, ni mwimbaji pia mtunzi wa nyimbo kutoka nchini Tanzania. Hapo awali alisainiwa na (King Kaka Records) mnamo mwaka 2016, rekodi ya lebo iliyoanzishwa na rapa wa Kenya King Kaka, na baadaye kujiunga na kikundi cha WCB Wasafi.[1][2] Baadhi ya nyimbo zake zinazofahamika zaidi ni pamoja na Kokoro aliyomshirikisha msanii Diamond Platnumz, Rudi aliyomshirikisha Patoranking, Show Me aliyomshirikisha Harmonize, na Bad Boy akishirikiana AY. Mnamo mwaka 2020 alitoa E.P yake ya kwanza, MiniTape kama msanii wa kujitegemea.

Maisha yake[hariri | hariri chanzo]

Anajulikana kwa kuwa faragha sana kuhusu maisha yake binafsi. Iliporipotiwa kuwa anatoka kimapenzi pamoja na msanii mwenzake wa Tanzania Lulu Diva mwaka 2020 aliziondoa haraka tetesi hizo.[3][4]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Rich Mavoko wins big against Diamond's Wasafi record". Ghafla.com. 10 August 2018. Iliwekwa mnamo 10 January 2021.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  2. "Tanzanian star Rich Mavoko leaves Kaka Empire for Diamond's label". Standardmedia.co.ke. 11 October 2017. Iliwekwa mnamo 10 January 2021.  Unknown parameter |url-access= ignored (help); Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  3. "I am not in a relationship with Lulu Diva". Standardmedia.co.ke. 16 August 2020. Iliwekwa mnamo 10 January 2021.  Unknown parameter |url-access= ignored (help); Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  4. "Lulu Diva 10 photos of Rich Mavoko's hot girlfriend". Pulselive.co.ke. 3 April 2018. Iliwekwa mnamo 10 January 2021.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Rich Mavoko kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.