Lavalava (mwanamuziki)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Lavalava (jina halisi Abdul Iddi; alizaliwa 27 Machi 1993) ni msanii kutoka lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) inayomiliki wasanii wengine kama Rayvanny, Queen Darleen,Zuchu,Mbosso na Diamond Platnumz ambaye ndiye bosi wa lebo hiyo.

Lavalava ni miongoni mwa vijana wanaofanya vyema kwenye muziki wa Bongo Fleva kwa sasa.Alijiunga WCB mwaka 2015 lakini alijulikana rasmi 22 May 2017.

Maisha ya muziki[hariri | hariri chanzo]

Safari yake ya muziki ilianzia mtaani kwao, Bunju, Dar es Salaam ambapo alijenga jina lake kwa kuimba nyimbo za watu kiasi kwamba asipokuwepo mtaani hapo pengo lake huonekana.

Lavalava alitoroka shule na kwenda THT kwa ajili ya kuimba, baada ya kupita kwenye mchujo wa wasanii wachanga zaidi ya 1000 na kuingia 50 bora, alifanya mafunzo ya muziki THT kwa miaka mitano na kukabidhiwa cheti cha masuala ya muziki na kupewa ruhusa ya kuingia mtaani kusaka au kutafuta menejimenti.