Nenda kwa yaliyomo

Mbosso

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mbwana Yusuph Kilungi (anajulikana kwa jina lake la kisanii kama Mbosso; amezaliwa 3 Oktoba 1991) ni mwimbaji, mtunzi na mwanamuziki kutoka nchini Tanzania.

Umaarufu ulianza akiwa na kundi zima la Yamoto Band ambalo ndani yake kuliwa na Aslay, Beka Flavour, Enock Bella na Mbosso. Kwa pamoja walikuwa wanaunda Yamoto Band chini ya Mkubwa Fella na Wanawe. Jina la Mkubwa na Wanawe lilikuwa na hadi sasa bado lipo hivyo hivyo kama Mkubwa na Wanawe. Ndani ya mkubwa na Wanawe kuna vipaji mbalimbali.

Baada ya Yamoto Band kufa, Mbosso aliamua kurudi nyumbani kwao kijijini huko Kibiti. Ambapo alijihusisha na vitendo mbalimbali vya kihalifu hasa kwa kukata tamaa na kuona wenzi wake wakiwa wanapata mafanikio yeye akiwa amebaki tu nyumbani. Jambo hili, lilikuwa tofauti kidogo na kina Aslay na Beka Flavour. Hawa waliendelea kutamba katika muziki hadi hapo Diamond Platnumz alipoona muda huu unafaa sasa kumrudisha Mbosso katika tasnia ya muziki kama alivyomuahidi mnamo mwakwa 2014 ya kwamba atamsaidia na kumuweka kwenye ramani ya muziki wa Bongo Flava. Wimbo wa kwanza wa Mbosso ulitoka mnamo tarehe 28 Januari 2018 na ulikwenda kwa jina la Watakubali.[1]

29 Januari alitambulishwa mbele ya hadhira ya kwamba yeye ni msanii kamili aliyesaini mkataba na WCB.[2]

Hadi sasa Mbosso ametoa wimbo kama vile Watakubali, Nimekuzoea, Alele, Shida, Picha Yake, Hodari, Nipepe, Hodari, Tamu. Wimbo mwingine aliotoa na kundi la Wasafi jina lake lilikuwa Zilipendwa na wimbo mwingine aliotoa na Diamond Platnumz na lavalava wimbo ambao jina lake ni Jibebe.

  1. Mbosso (2018-02-04), Life of Mbosso (Historia ya Maisha ya Mbosso), iliwekwa mnamo 2018-09-19
  2. Smash Juanito (2018-02-08). "MBOSSO AANZA NA MAFANIKIO WCB WIMBO MMOJA TU AWEA REKODI | Smash Juanito". MBOSSO AANZA NA MAFANIKIO WCB WIMBO MMOJA TU AWEA REKODI | Smash Juanito. Iliwekwa mnamo 2018-09-19.
Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mbosso kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.