Nenda kwa yaliyomo

Aslay Isihaka Nassoro

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Aslay)
Aslay
Jina la kuzaliwaAslay Isihaka Nassoro
Amezaliwa6 Mei 1995 (1995-05-06) (umri 29)
Kazi yakeMwimbaji
AlaSauti

Aslay Isihaka Nassoro (maarufu kama Dogo Aslay; alizaliwa 6 Mei, 1995) ni msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka Tanzania.

Alianza kufahamika kuanzia mwaka 2011 baada ya kutoa kibao chake cha Nakusemea alichokitoa akiwa chini ya Mkubwa Fella. Kabla ya hapo, alitoa wimbo mwingine uitwao Niwe Nawe akiwa amemshirikisha Temba. Baadaye akatoa nyimbo nyingine kadhaa kabla ya kujiunga na bendi ya vijana ya Yamoto Band.

Akiwa ndani ya bendi hiyo, alionesha uwezo mkubwa wa kuimba, akiwa na wenzake, Beka Flavour, Maromboso na Enock Bella. Nyimbo alizoshiriki kutunga na kuimba akiwa Yamoto Band ni pamoja na Yamoto (Nitajuta), Cheza Kwa Madoido, Mama, Nisambazie Raha na nyingine nyingi.

Yamoto Band haikudumu sana ambapo ilianza 2013/2014 hadi 2017 ilipovunjika kwa sababu mbalimbali na wasanii waliokuwa kwenye kundi hilo kuanza kufanya kazi zao kwa kujitegemea. Kuanzia 2017, Aslay akiwa msanii wa kujitegemea chini ya meneja wake wa zamani, Chambuso, alianza upya kung'ara.[1]

Akiwa msanii wa kujitegemea, ametoa nyimbo nyingi mfululizo hali ambayo imechanganya wengi, lakini mwenye alielezea kwanini amefanya ni kwa sababu hana nyimbo nyingi alizofanya akiwa msanii wa kujitegemea zaidi ya zile alizokuwa na Yamoto Band[2]

Ili asiimbe za Yamoto akiwa kwenye matamasha, kaamua kutoa nyimbo nyingi. Nyimbo hizo ni pamoja na Angekuona, Usiitie Doa akiwa na Khadija Kopa, Muhudumu, Baby, Likizo, Pusha Natamba na Huna. Awali ilitazamika kama Mkubwa Fella ndiye hasa mmiliki wa muziki wa kizazi kipya, lakini kupitia Aslay, Chambuso anasema si lazima yeye ndiye awe meneja bora wa muziki huu.[3]

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. MENEJA CHAMBUSO AIKACHA MKUBWA NA WANAWE AUNGANA NA ASLAY KUBORESHA LABEL MPYA
  2. "Aslay Songs: Download New Aslay Songs 2019 & 2018, lyrics and video Mp3TINA Magazine". TINA Magazine (kwa Kiingereza (Uingereza)). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-09-26. Iliwekwa mnamo 2019-03-07.
  3. CHAMBUSO: MUZIKI SIYO WA MKUBWA FELLA Ingizo la September 21, 2017 na Global Publishers.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Aslay Isihaka Nassoro kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.