Watakubali

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
“Watakubali”
“Watakubali” cover
Kasha la Watakubali
Single ya Mbosso
Imetolewa 28 Januari, 2018
Muundo Upakuzi wa mtandaoni
Imerekodiwa 2017/2018
Aina Bongo Flava
Urefu 3:47
Studio Wasafi Records
Mtunzi Mbosso
Mtayarishaji Laizer Classic
Mwenendo wa single za Mbosso
"Watakubali"
(2018)
"Nimekuzoea"
(2018)

Watakubali ni jina la wimbo uliotungwa na mwimbaji/mwanamuziki wa Bongo Flava kutoka nchini Tanzania - Mbosso. Wimbo umetoka tarehe 28 Januari 2018.[1] Huu ni wimbo wa kwanza kutoka tangu aingie mkataba na WCB Wasafi. Wimbo umetayarishwa na Laizer Classic.[2]

Wimbo unamzungumzia kijana mmoja anayependwa na mwanamke mwenye uwezo kuliko yeye. Mbaya zaidi, Mbosso hana pesa, hana ajira wala hana elimu ya kutosha vigezo vya mwanamke huyo. Pamoja na kasoro zote hizo, bado yule mwanamke anaonesha kumpenda Mbosso kwa hali aliyonayo. Katika wimbo anaelezea pia kisa kibaya alichowahi kuwafanya wazee wa mwanamke anayempenda. Je, kwa tukio la kukuba ukweni, watakubali?

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Mbosso (2018-01-28), Mbosso - Watakubali (Official Video), retrieved 2018-09-23 
  2. "Audio | Mbosso – Watakubali | Mp3 Download - The Choice", The Choice (in en-US), 2018-01-28, retrieved 2018-09-23