Lava Lava (mwimbaji)
Lava Lava | |
---|---|
Jina la kuzaliwa | Abdul Juma Idd |
Amezaliwa | Machi 27, 1993 (umri 30 ) |
Kazi yake | mwanamuziki |
Abdul Juma Idd (maarufu kwa jina lake la kisanii Lava Lava[1]; amezaliwa 27 Machi 1993) ni mwimbaji anayetokea Tanzania aliyesajiliwa chini ya lebo ya muziki WCB Wasafi[2][3] inayomiliki wasanii wengine kama D voice, Queen Darleen,Zuchu,Mbosso na Diamond Platnumz ambaye ndiye mmiliki wa lebo hiyo.
Lavalava ni miongoni mwa vijana wanaofanya vyema kwenye muziki wa Bongo Fleva kwa sasa. Alijiunga 'WCB mwaka 2015 lakini alijulikana rasmi.
Maisha ya muziki
[hariri | hariri chanzo]Safari yake ya muziki ilianzia mtaani kwao, Bunju, Dar es Salaam ambapo alijenga jina lake kwa kuimba nyimbo za watu kiasi kwamba asipokuwepo mtaani hapo pengo lake huonekana.
Lavalava alitoroka shule na kwenda Tanzania House of Talents (kifupi: THT) kwa ajili ya kuimba, baada ya kupita kwenye mchujo wa wasanii wachanga zaidi ya 1000 na kuingia 50 bora, alifanya mafunzo ya muziki kwa miaka mitano na kukabidhiwa cheti cha masuala ya muziki na kupewa ruhusa ya kuingia mtaani kusaka au kutafuta menejimenti.
Baada ya kumaliza masomo yake aliomba nafasi WCB Wasafi na kubahatika kusajiliwa.[4]
Diskografia
[hariri | hariri chanzo]Albamu
- Promise
Nyimbo
- Saula akishirikiana na Harmonize
- Warembo akishirikiana na Susumila
- Niue
- Gundu
- Teja
- Tuachane
- Habibi
- Jibebe akishirikiana na Mbosso na Diamond Platnumz
- Hatuachani
- Tukaze Roho
- Utatulia
- Utanipenda cover
- Go gaga
- Wanga
- Tekenya
- Corona
- Bachela
- Single
- Nimekuchagua
- Dede
- Tattoo
- Balaa
- Ya Ramadhan
- Kizungu zungu
- Dondosa
- Maji
- Kibango
- Mama Samia
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Sonko gives Wasafi singer Lava Lava extensive tour of his massive shoe closetInterview". K24tv (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-12-09.
- ↑ "WCB's Lava Lava hits new YouTube Milestone & he is over the Moon closetInterview". Pulselive (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-07-07.
- ↑ "Singer Lava Lava clears the air on exiting Wasafi records". The Standard Media (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-08-30.
- ↑ "Diamond's Wasafi Signee, Lava Lava Faints On Stage After Getting A Kiss From A Fan (Video)". Kahawa Tungu (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2018-07-30.
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Lava Lava (mwimbaji) kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |