Zuchu
Zuhura Othman Soud (anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii Zuchu; alizaliwa tarehe 22 Novemba mwaka 1993[1]) ni mwanamuziki, mtunzi wa nyimbo na msanii wa kurekodi wa Kitanzania aliezaliwa Zanzibar. Ni mhamasishaji na muendelezaji mzuri wa mtindo mpya wa muziki unaoitwa Singeli. Nyimbo yake ya 'Hujanizidi' inadhihirisha jambo hili. Nyimbo zake nyingi ziko kwenye mtindo wa Singeli. Hivyo basi, tunaweza kumuita Malkia wa Singeli. Amesainiwa chini ya lebo ya WCB Wasafi Records chini ya uongozi wa Diamond Platnumz.[2][3][4]
Alitunukiwa tuzo ya silver play button na mtandao wa kijamii wa Youtube kwa kuwa msanii wa kwanza wa kike Afrika ya mashariki kwa kufikisha wafuasi zaidi ya 100,000 ndani ya wiki moja.[5]
Katika wiki ya kusheherekea siku ya kuzaliwa, Zuchu alitunukiwa tuzo ya msanii bora chipukizi wa mwaka 2020 na tuzo All Africa Music Awards AFRIMMA.[6]
Maisha ya awali
[hariri | hariri chanzo]Zuchu amezaliwa kwenye familia ya wanamuziki. Ni binti wa mwanamuziki wa taarabu anayefahamika kwa jina la Khadija Kopa.[7][8][9][10] Zuchu alianza kuimba akiwa na umri mdogo na baadae kushirikiana na mama yake Khadija Kopa katika wimbo unaofahamika kama Mauzauza [11]
Zuchu alitambulika rasmi kwenye Tasnia ya muziki mnamo Aprili 2020.[12] Mpaka sasa ana albamu moja na alichaguliwa kushiriki mashindano ya kuwania tuzo ya MTV MAMA awards ya mwaka 2021. Kwenye mashindano hayo, Zuchu alipangwa katika kipengele cha 'best breakthrough act', na alikabiliwa na ushindani kutoka kwa Elaine na Focalistic wa Afrika Kusini na Tems na Omah Lay wote kutoka Nigeria, John Blaq (Uganda) na Sha Sha (Zimbabwe).[13]
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Zuchu alianza kuimba akiwa na umri mdogo na baadaye alishirikiana na mama yake, Khadija Kopa, katika wimbo ulioitwa Mauzauza uliomo kwenye EP yake ya kwanza I am Zuchu. Mara ya kwanza kujitokeza hadharani kama msanii ilikuwa mwaka 2015. Alitumbuiza miongoni mwa wasanii wengine katika toleo la kwanza la TECNO OWN THE STAGE lililofanyika Lagos, Nigeria[14], ambapo alifanya majaribio (audition) pamoja na msanii wa Tanzania, Nandy.
Mwaka 2022, Zuchu alikua msanii wa kike mwenye idadi kubwa zaidi ya wanaojisajili (subscribers) kwenye YouTube katika eneo la Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara[15]. Miezi michache baadaye, alikua msanii wa kwanza wa kike katika Afrika Mashariki kufikisha jumla ya mitiririko (streams) milioni 100 kwenye jukwaa la Boomplay.[16]
Vilevile mwaka 2022, Zuchu alikua msanii wa kwanza wa kike kutoka Afrika Mashariki kupata uteuzi (nominashion) katika tuzo za MTV EMAs.[17]
Zuchu alianza mwaka 2023 kwa kutoa wimbo mpya ulioitwa Utaniua. Wimbo huo ulipokelewa vizuri na wakosoaji wa muziki, ambapo mwandishi wa habari za muziki nchini Tanzania, Charles Maganga, aliusifu wimbo huo kama kazi ya karibu kihisia inayotoa heshima kwa muziki wa Bongo Flava na Baibuda.[18]
Mnamo Machi 2023, Zuchu alitoa video yake ya kwanza rasmi ya muziki kwa mwaka 2023 kwa wimbo ulioitwa Napambana.[19]
Mwezi Juni 2023, Zuchu alitangaza kufikisha jumla ya watazamaji zaidi ya milioni 500 kwenye YouTube, na hivyo kuwa msanii wa kwanza wa kike Afrika Mashariki na wa tano kwa ujumla barani Afrika kufikia rekodi hiyo.[20]
Mwaka 2023 pia, wimbo wa Zuchu wa mwaka 2021 ulioitwa Sukari uliorodheshwa katika nafasi ya nane na Notjustok kwenye orodha yao ya nyimbo bora za Tanzania za muongo mmoja kuanzia 2012 hadi 2022.[21]
Diskografia
[hariri | hariri chanzo]Albamu
[hariri | hariri chanzo]Zuchu aliachia albamu ya kwanza iliyotambulika kama “I am Zuchu“ mwaka 2020 ikiwa na nyimbo 7. [22] Albamu yake ndiyo albamu iliyosikilizwa na watu wengi zaidi nchini Tanzania kwa mwaka 2020 na video za nyimbo zake zimetazamwa na mamilioni ya watu. Mwanamziki Zuchu kwa sasa anatamba na albamu yake mpya iitwayo Peace And Money yenye nyimbo kama Till I Die akiwa ame mshirikisha Spyro, Lollipop akiwa amemshirikisha Yemi Alade, Mwizi, Antenna, Makonzi, Lullaby akiwa na Majeeed, I Don't Care, Mama, Nimechoka akiwa amemshirikisha msani mkubwa Tanzania Diamond. [23]
Nyimbo zake
[hariri | hariri chanzo]| Mwaka | Nyimbo | Albamu |
|---|---|---|
| 2020 | "Hakuna Kulala" | I Am Zuchu EP |
| "Nisamehe" | ||
| "Kwaru" | ||
| "Wana" | ||
| "Raha" | ||
| "Ashua"(feat. Mbosso) | ||
| "Tanzania ya Sasa" | ||
| "Shangilia" | ||
| "Mauzauza"(feat. Khadija Kopa) | ||
| "Cheche" (feat. Diamond Platnumz) | ||
| "Litawachoma" (feat. Diamond Platnumz) | ||
| "Hasara" | ||
| "Nobody" (feat. Joeboy) | ||
| 2021 | "Sukari" | |
| Mwaka | Nyimbo | Albamu |
|---|---|---|
| 2024 | "Till I Die"(feat. Spyro) | Peace and Money |
| "Lollipop"(feat. Yemi Alade) | ||
| "Mwizi" | ||
| "Antenna" | ||
| "Makonzi" | ||
| "Lullaby"(feat. Majeed) | ||
| "I Don't Care" | ||
| "Cherie"(feat. Lava Lava) | ||
| "Tinini"(feat. H-art The Band) | ||
| "Mama" | ||
| "Nimechoka" | ||
| "Wale wale"(feat. Diamond Platnumz) | ||
| "Hujanizidi" (feat. D Voice) | ||
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Zuchu – YouTube". www.youtube.com. Iliwekwa mnamo 6 Novemba 2020.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Zuchu Bio – Age, Career, Education, Songs, WCB, Boyfriend, Net Worth". www.eafeed.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 3 Juni 2020.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Zuchu is the new face on Diamond's record label WCB". The Citizen. Iliwekwa mnamo 4 Juni 2020.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Zuchu set to rise under the auspices of Diamond Platnumz". Music in Africa (kwa Kiingereza). 17 Julai 2020. Iliwekwa mnamo 6 Novemba 2020.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Zuchu set to rise under the auspices of Diamond Platnumz". Music in Africa (kwa Kiingereza). 17 Julai 2020. Iliwekwa mnamo 6 Novemba 2020.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Check out full list of winners at the 2020 AFRIMMA Awards". Pulse Live Kenya (kwa American English). 16 Novemba 2020. Iliwekwa mnamo 24 Novemba 2020.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Diamond's new signee Zuchu features her mum, legendary Khadija Kopa, in new song days after joining WCB". TUKO. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-03-02. Iliwekwa mnamo 10 Juni 2020.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Kati ya wasanii hawa mmoja atajiunga WCB". Mwananchi. Iliwekwa mnamo 10 Juni 2020.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Diamond's new signee Zuchu features her mum, legendary Khadija Kopa, in new song days after joining WCB". TUKO. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-03-02. Iliwekwa mnamo 10 Juni 2020.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Kati ya wasanii hawa mmoja atajiunga WCB". Mwananchi. Iliwekwa mnamo 10 Juni 2020.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "ZUCHU – Biography – Age, Family, Early life, Record Label, Music, Net Worth". Daily4mative. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-03-04. Iliwekwa mnamo 2021-03-06.
- ↑ "Why WCB's new signee Zuchu is a force to reckon with as she unveils her EP 'I am Zuchu'". Pulselive. Iliwekwa mnamo 10 Juni 2020.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-02-25. Iliwekwa mnamo 2021-03-06.
- ↑ EP4 Zouchu Performance (kwa Kiingereza), iliwekwa mnamo 2021-03-14
- ↑ admin (2022-10-25). "Zuchu the most Youtube subscribed female artist in Sub-Saharan Africa — citiMuzik" (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2023-02-21.
- ↑ "Diamond, Zuchu, Harmonize and Nandy emerge top artists in Boomplay Recap 2022". The Citizen (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2023-02-21.
- ↑ "Tanzanian singer Zuchu nominated for 2022 MTV Awards | The East African". www.theeastafrican.co.ke. Iliwekwa mnamo 2024-01-01.
- ↑ "Zuchu Drops A Brand New Song Titled "Utaniua" | Notjustok". Latest East African & Bongo Flava Music, Songs & Video - Notjustok (kwa American English). 2023-02-10. Iliwekwa mnamo 2023-02-21.
- ↑ "Zuchu - Napambana (Official Music Video)". Nyimbo Mpya (kwa American English). 2023-02-10. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-03-06. Iliwekwa mnamo 2023-03-06.
- ↑ "@officialzuchu surpassed 500M total views on youtube, She is the 1st Female Artist To Surpass This Milestone In East Africa & 5th in All Africa". Facebook (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2023-06-29.
- ↑ "Tanzanian singer Zuchu nominated for 2022 MTV Awards | The East African". www.theeastafrican.co.ke. Iliwekwa mnamo 2024-01-01.
- ↑ "Zuchu: I Am Zuchu". deezer.com.
- ↑ https://www.thecitizen.co.tz/tanzania/news/entertainment/zuchu-named-on-bbc-s-10-african-musicians-to-look-out-for-in-2021-3245486