Khadija Kopa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Khadija Kopa
Jina la kuzaliwaKhadija Omar Abdallah Kopa
Amezaliwa1963
Kazi yakeMwimbaji, mtunzi wa nyimbo, Mtayarishaji wa rekodi, mwanamuziki
AlaSauti
Miaka ya kazi1990–hadi sasa
Ameshirikiana naDiamond Platnumz, Abdul Misambano, Ali Star, Mzee Yusuph, TOT

Khadija Omar Abdallah Kopa (amezaliwa 1963 huko Zanzibar) ni mwimbaji wa muziki wa Taarab, mtunzi wa nyimbo na mfanyabiashara kutoka nchini Tanzania. Anafahamika zaidi kwa ushirikiano wake mkubwa na bendi ya TOT. Ameanza kuimba Taarab tangu 1990 na bendi ya kwanza kujiunga nayo ilikuwa Culture Musical Club.

Maisha na kazi[hariri | hariri chanzo]

Khadija Kopa alizaliwa mwaka 1963 kisiwani Zanzibar na ni mtoto wa kipekee katika familia ya Kopa. Ameolewa na ana watoto wanne na wajukuu wawili. Kazi ya sanaa alianza mwaka 1990 katika Kikundi cha Culture Musical Club. Mbali ya muziki, Kopa ni mama wa nyumbani, mfanyabiashara na pia mwanaharakati wa kisiasa nchini Tanzania. Khadija alikuwa akipenda kuimba tangu akiwa mdogo, akisomea madrasa Zanzibar. Akiwa chuoni (madrasa) alikuwa msomaji mzuri wa qaswida, halafu vilevile alipokuwa Young Pioneer, alikuwa kwenye kikundi cha kwaya. Halkadhalika Shuleni alikuwa kwenye mambo ya ngoma, mambo ya utamaduni na kwaya. Shule yao ilikuwa bingwa kwa kwaya Zanzibar. Aliendelea hivyo hadi katika shule ya upili.

Siku moja alikuwa amekaa huku akiiga wimbo. Akapita babu yake aliye katika kikundi cha Culture Musical Club cha Zanzibar. Akamsifia ya kwamba anajua kuimba. Basi akachukua hatua ya kuandika barua kwa niaba yake bila ya kumshauri, akaipeleka Culture Musical Club kuomba ajiunge nao.

Khadija pia amepata kushirikiana na waimbaji wengine wa kike kama vile Mwanamtama Amir, marehemu Leila Khatib na wanaume kama akina Abdul Misambano na Ali Star, waliporomosha nyimbo ambazo zilitamba miaka hiyo katika ulimwengu wa Taarab.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Musical notes.svg Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Khadija Kopa kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.