Tmk Wanaume Halisi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kikosi cha Tmk Wanamume Halisi.

Tmk Wanaume Halisi ni kundi la muziki wa Rap na Hip Hop ya Bongo linalotokea wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam Tanzania.

Ni kundi linaloundwa na wasanii mahili wa muziki huu wa hip hop na bongo flava, kinala wa kundi hilo ni msanii machachali, mwelevu, Juma Nature akiwa na wasanii wengine kama vile Rich One, Doro, D Chief, Inspector Haroun, Mzimu, Luteni Karama, na wengine wengi tu.

Labda kwa kurahisisha unaweza kusema kwamba kundi hili ni muungano wa makundi matatu yaliyowahi kufanya vizuri na jitihada zao unaweza kusema ndizo zilizoweza kuufikisha muziki huu hapa walupofika hii leo.

Makundi haya tunayoyazungumzia ni Gangwe Mobb linalojumuisha naLuteni Karama,Wachuja Nafaka linalojumuisha na Juma Nature na Doro, kundi lingine ni Gangsters with Matatizo (GWM) linalowakilishwa na D-Chief.

Musical notes.svg Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tmk Wanaume Halisi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.