Nenda kwa yaliyomo

Gangwe Mobb

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Gangwe Mobb
Gangwe Mobb upande wa kushoto (Inspector Haroun kainamia meza anaandika) na wa mbele yake Dogo Side, na G.W.M. upande wa kulia (D-Chief kushoto na KR Mullah kulia). Wakati wa tamasha la Mwaka Elfu Mbili lililoandaliwa na Madunia Foundation mnamo tarehe 9 Mei, 1999

Gangwe Mobb ni kundi la muziki wa hip hop ya Kitanzania. Kundi linatokea katika maeneo ya Temeke Mikoroshini huko mjini Dar es Salaam. Kundi linaunganishwa na wanachama wawili ambao ni: Inspector Haroun (jina kamili ni Haroun Kahena) na Luteni Karama (Karama Bakari). Kundi hili lilianzishwa mwishoni mwa miaka ya 90 punde baada ya Kwanza Unit, Mr. II na wengineo waliosababisha muziki wa hip hop wa Kiswahili nchini Tanzania kujipatia umaarufu. Jina la "Gangwe" linatokana na istilahi ya neno la msimu mashuhuri la Kiingereza la miaka ya 80 "hardcore". Ki-muktadha, gangwe inalenga hasa uhalisia wa hip hop ya watu wa mtaani ambamo mara nyingi wanaimba kwenye nyimbo zao. [1]

Kibao chao cha kwanza mashuhuri kilikuwa "Mauzauza". Albamu yao ya kwanza, "Simulizi la Ufasaha" ikiwa imejumlisha vibao vikali ambavyo ni "Ngangali" na "Mtoto wa Geti Kali". Albamu yao ya pili ni "Nje Ndani", ilitolewa mnamo mwaka wa 2002 ilikuwa na kibao chake kilicholeta gumzo, "Asali wa Moyo". Miongoni mwa single zao walipata kuziita "Bundasiliga" ambazo zilikuwa zikitoa ujumbe kwa jamii. [2] Pia wamewahi kushirikiana na kundi la Kikenya la Necessary Noize kwenye kibao cha "Tunajirusha".

Gangwe Mobb wanaeleza kwamba muziki wao kama rap katuni. Inaelezea kuhusu hali halisi ya maisha ya watu hali chini jinsi wanavyo-haha katika kujitafutia riziki ya kila siku. Nyimbo zao pia zinajulikana kwa kuanzisha lahaja mpya ya maneno ya msimu kwa kila nyimbo yao.[3]

The group has a song named "Rap Katuni" on their "Nje Ndani" album.

Mwaka wa 2004 kwenye Tuzo za Muziki Tanzania albamu ya Nje Ndani ilipata kuchaguliwa kama Albamu Bora ya Hip Hop.[4]

Kundi limetengana tangu mwaka wa 2004. Tangu hapo, Inspekta Haroun ameanza kazi kama msani wa kujitegemea, wakati Luteni Kalama amefunikwa vibaya-vibaya lakini alipata kuwa na kundi la Wanaume Family ambalo lilikuwa likiongozwa na Juma Nature. Mwaka wa 2008 Gangwe Mobb wametangaza kurudi[5].

Walisema kwamba jina lao linatokana na kundi kongwe la hip hop la Mobb Deep.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Kenya, Uganda&Tanzania". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-10-10. Iliwekwa mnamo 2010-11-20. {{cite web}}: Unknown parameter |= ignored (help)
  2. Mueller, Gavin. "Bongoflava: The Primer." Stylus Magazine, 12 Mei 2005. [1] Archived 8 Januari 2011 at the Wayback Machine.
  3. Out|here records - bongoflava - African hiphop label, African rap label, African reggae label, African ragga label, African dancehall label
  4. "Tanzania Music Awards - Nominees 2004". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2004-12-04. Iliwekwa mnamo 2004-12-04.
  5. Darhotwire.com: Gangwe is Back! Archived 26 Oktoba 2008 at the Wayback Machine.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]