Master Jay

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Joachim Kimario
Jina la Kiraia Joachim Kimario
Jina la kisanii Rap Master Jay, Master Jay, Baba Nuru nk.
Nchi Tanzania
Alizaliwa 8 Agosti 1973
Aina ya muziki Hip Hop, Bongo Flava, Kwaya, Dansi
Kazi yake Mtayarishaji
Miaka ya kazi mn. 1995 -
Ameshirikiana na P Funk, Bonny Luv,Rajabu Marijani, Bizz Man, Marco Challi nk.
Ala Kinanda,Guitar, Kinakilishi, Kuunjini Sauti
Kampuni Mj Records

Joachim Kimario (Master Jay) ni muandaaji wa muziki nchini Tanzania Master Jay alizaliwa Tar. 8 Agosti mwaka 1973 akiwa mtoto pili katika familia ya marehemu Mzee Sylvan Kimario na mama yake Scholastica Kimario ambaye kwa sasa ni afisa wa UNDP nchini Lesotho ambapo dada yake Catherine Kimario yeye anaishi nchini Kossovo akiwa kama mfanyakazi wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini humo.

Master ambaye pia amewahi kupata tuzo ya Kili Music Awards mara mbili, mwaka 2004 na 2007. Master Jay ana uwezo mkubwa sana wa utengenezaji wa muziki. Anamiliki studio tatu tofauti, moja ya muziki wa Kwaya, moja ya Bongo Flava na nyingine ya muziki wa Dansi.

Elimu[hariri | hariri chanzo]

Master Jay alipata elimu ya msingi katika shule ya msingi Upanga lakini aliishia darasa la tano na kuhamishiwa Botswana baada ya familia yake kuhamishiwa nchini huko kikazi.

Ilivyofika mwaka 1989 alipata digrii ya electronics katika chuo kimoja kilichopo bara Ulaya mbali na shughuli za kimuziki.

Muziki na Vikwazo vya Kifamilia[hariri | hariri chanzo]

Baada ya kupata dirii yake alirudi nyumbani na kuendelea na shughuli zake za kawaida pamoja na muziki, baba yake hakutaka kabisa mwanae ajishughulishe na muziki kiasi kufikia kutaka kumuachia radhi.

Pamoja na Vikwazo alivyopewa na baba yake mzazi, Master Jay hakuacha muziki kwa kudai kuwa mzuki upo ndani ya damu yake.

Studio Rasmi[hariri | hariri chanzo]

Mnamo mwaka 1996 Master Jay aliamua kujishulisha kabisa na maswala ya Utengezaji wa muziki kwa kuamua kuanzisha rasmi studio yake aliyoipa jina lake la "Mj Production" japokuwa babake alikuwa haja ridhia hilo. Baadae akatoa wimbo wa kundi la Kwanza Unit na baada ya muda kidogo tena akatoa nyimbo ya kundi la 4 Crews Flavour, baada ya hapo ndipo mzee wake alipoanza kuoynesha moyo na kuanza kukubali Anachofanya na hii ilinipa moyo wa kufanya kazi kwa bidii zaidi.