Dansi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Wakinamama kucheza ngoma huko Nairobi.

Dansi (kutoka Kiingereza dance) ni tendo la kufanya miendo ya mwili sambamba na mipigo au mahadhi ya muziki.

Katika utamaduni wa Kiafrika dansi huwa kwa kawaida na umbo la kucheza ngoma, yaani ngoma ni ala ya kutawala miendo.

Lakini katika tamaduni nyingine za dunia muziki wa dansi unatolewa kwa kutumia ala nyingine kama filimbi au zeze.

Leo hii kila aina ya muziki hutumiwa kwa kucheza dansi.

Dansi huwa na pande nyingi. Inaweza kutokea kama mchezo wa kijamii, michezo, sanaa, aina ya tiba, namna ya kuonyesha hisia au pia ibada.