Filimbi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Filimbi mbalimbali
Filimbi za kuungwa
Filimbi ya Kihindi ikipigwa kutoka pembeni


Filimbi ni ala ya muziki inayopatikana kote duniani. Ina umbo la bomba na hewa inapulizwa ndani kwa mdomo kupitia shimo; mkondo wa hewa unapita kwenye kona kali ambako unaanza kutingatinga ukisababisha nguzo ya hewa iliyopo ndani ya bomba la filimbi kutingatinga pia; mitetemo hii ni sauti ya filimbi.

Urefu wa bomba unafanya tabia ya sauti; kama filimbi ni fupi inatoa sauti ya juu; kama filimbi ni ndefu ina sauti ya chini.

Filimbi nyingi huwa na mashimo kanda yanayofunikwa na kufunguliwa kwa vidole. Kwa kufungua shimo mchezaji anafupisha au kurefusha nguzo ya hewa ndani ya filimbi inayotingatinga na kubadilisha sauti hivyo.

Kuna muundo kadhaa:

  • shimo la kupulizia liko upande wa pembeni wa filimbi
  • shimo liko mwanzoni wa bomba la filimbi
  • kuna bomba moja lenye mashimo ya pembeni kwa kubadilisha sauti
  • kuna mabomba bila mashimo ya pembeni yaliyounganishwa pamoja; kila filimbi ina sauti yake na mchezaji anateleza mdomo wake juu ya mashimo ya mabomba akipiga muziki yake.