Hakimu
Mandhari
(Elekezwa kutoka Jaji)
Hakimu ni mtu anayeendesha kesi mahakamani akiwa peke yake au akiwa kama sehemu ya jopo la mahakimu.
Mamlaka, kazi njia ya uteuzi, nidhamu na mafunzo ya mahakimu yanatofautiana katika mahakama mbalimbali.
Hakimu anatakiwa kuendesha kesi bila kuonyesha upendeleo na katika mahakama ya wazi. Hakimu anasikiliza mashahidi na ushahidi uliowasilishwa na mawakili wa kesi, kisha kutathmini ukweli na hoja za pande mbili tofauti, na hatimaye anatoa uamuzi juu ya suala hilo kulingana na tafsiri yake ya sheria na hukumu yake binafsi.
Katika baadhi ya mahakama, mamlaka ya hakimu inaweza kuwa sawasawa na ya jopo la majaji. Katika mifumo ya uchunguzi wa tuhuma hakimu anaweza pia kuwa hakimu mpelelezi.
Makala hii kuhusu mambo ya sheria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Hakimu kama historia yake au uhusiano wake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |