Waidakho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

WAIDAKHO[hariri | hariri chanzo]

Waidakho, ni miongoni mwa kabila ndogo za kabila la Abaluhya wanaokalia eneo la rotuba nyingi la Wilaya ya Kakamega, Mkoa wa Magharibi nchini Kenya. Eneo wanalokalia Waidakho inajulikana kiutawala kama Ikolomani, Ikolomani likiwa ndilo jimbo la uchaguzi la kipekee katika eneo hili.

Kama ilivyo na kawaida katika maeneo ya Mkoa wa Magharibi , eneo la Idakho, Kakamega lina wingi wa wakaazi huku makadirio ya idadi ya wakaazi mwaka wa 2oo7 yakiwa yamezidi watu 150,000.

Inaaminika kuwa Waidakho ni wazaliwa wa Mwitakho.[1]

Upungufu wa mashamba na utandawazi umewalazimu Waidakho kubadili mtindo wao wa maisha huku wengi wakijihusisha na ukulima wa ng'ombe za maziwa na katika kiwango kidogo,ukulima wa majani chai. Mhindi hata hivyo ndio mmea unaokuzwa zaidi,ukiwapa chakula chao cha kawaida -sima (ubushuma). Huvunwa mara mbili kwa mwaka.

Hata hivyo,hali yao ya kimaisha ya kitamaduni huwasaidia tu kuishi maisha yao ya kisasa.

Wengi wao wakiwa na kiwango fulani cha masomo(62%), Waidakho siku hizi wanajiusisha kwenye sekta za biashara,wafanyi kazi wa umma na sekta za kibinafsi kwenye miji mikuu ya Afrika Mashariki.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Mwidakho pamoja na kakake, Mwisukha wanaaminika kuwa waanzilishi wa kabila ndogo za - Idakho and Isukha.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Waidakho wanakalia eneo la Ikolomani,ambalo kwa sasa ni Wilaya ya Kakamega Kusini mji mkuu wake ukiwa Malinya,Magharibi mwa Kenya.

Sanaa na Utamaduni[hariri | hariri chanzo]

Vita vya Ng'ombe dume[hariri | hariri chanzo]

Licha ya kuwa mchezo wa kutumbuiza watu,pia ni sehemu ya mila zao ambapo hufanyika katika sherehe yeyote ya matanga na pia kwenye sherehe zingine za kitamaduni.Mchezo huu huusisha ng'ombe dume na hufanyika mathalani asubuhi na mapema.

Densi ya Isikuti[hariri | hariri chanzo]

Isukuti ni aina ya ngoma iliyoundwa kutoka kwa ngozi maalum.Densi ya Isukuti ni maarufu miongoni mwa jamii ya Abaluhya Waidakho wakiwemo.Densi hii huchezwa katika sherehe za kitamaduni kama vile matanga na harusi.Pia densi hii hutumika kusherehekea hasawa katika michezo kama vile kandanda.Mashabiki wa AFC Leopards,-timu ambayo inajumuisha Waluhya na iliyoanzishwa kwa misingi ya Uluhya-,hucheza Isukuti kwa kusgalia timu yao katika mechi za Ligi Kuu ya Kenya.

Lipala[hariri | hariri chanzo]

Lipala ni mtindo wa kucheza miongoni mwa jamii za Waluhya.Mtindo huu hujumuisha mchezaji kupiga makofi na kisha kushika kichwa chake na mkono mmoja huku mkono mwingine ukiwa kwenye kiuno huku akikitisa.

Lugha[hariri | hariri chanzo]

Lugha ya Waidakho ni Kiidakho.

Dini[hariri | hariri chanzo]

Hakuna dini maalum ya Waidakho.Hata huivyo,Ukristo ndio dini iliyoenea.Dhehebu ya Makweka-Friends- ndio maarufu.Madhehebu/makanisa mengine yaliyoko ni kama vile:Katoliki,PAG na Legio Maria miongoni mwa zingine.

Fasihi[hariri | hariri chanzo]

Fasihi yao inajumuisha nyimbo na densi kiutamaduni.Kuna hata hivyo fasihi za kisasa kama vile tamthilia na riwaya ambazo pia wanausikana nazo.

Kabila Ndogo za Waidakho[hariri | hariri chanzo]

Abashimuli Abashikulu Abamasaba Abashiangala Abamusali Abangolori Abamahani [2]

Viongozi wa sasa[hariri | hariri chanzo]

Hon. Dr. Bonny Khalwale, MP Ikolomani

==Marejeo==