Waturkana

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Turkana
TurkanaPeople.jpg
Turkana man with children in traditional Turkana clothing.
Total population
340,000
Regions with significant populations
Kaskazini-Magharibi ya Kenya
Languages

Kiturkana

Religion

dini ya asili, Ukristo

Related ethnic groups

Maasai

Waturkana ni watu wa asilia ya Nilote wa Kenya, idadi yao ikiwa karibu 340,000. Ni wakaazi wa Wilaya ya Turkana kaskazini magharibi mwa Kenya, eneo kame na kavu inayopakana na Ziwa Turkana upande wa mashariki. ,Kusinimwao kunaishi Wapokot (Wapökoot), Warendille, na Wasamburu. Lugha ya Waturkana, lugha ya asili ya Nilotes wa Mashariki, pia hujulikana kama Kiturkana; jina yao kwa lugha hii ni Ng'aturk(w)ana.

Waturkana wanajulikana kwa ajili ya kukuza ngamia na kushona vikapu. Katika fasihi simulizi zao, wao hujiita watu wa fahali ya kijivu , baada ya Zebu, ya ukuzaji wake ambao una nafasi muhimu sana katika historia yao. Katika miaka ya karibuni, mipango ya misaada ya maendeleo imelenga kuanzisha uvuvi miongoni mwa jamii ya Waturkana (ambayo ni mwiko katika jamii ya Waturkana) na kupata mafanikio mbalimbali.

Mavazi[hariri | hariri chanzo]

Kijadi, wanaume na wanawake wote huvaa mikanda iliyotengenezwa kutoka kwa ngozi ya mraba , lakini kila aina ya watu hujipamba kwa mapambo mbali mbali. Mara nyingi wanaume huvalia mikanda zao sawa na shuka mara nyingi upande mmoja ukishikana na mwingine kwenye bega lao la kulia, na hubeba visu vya mkononi vilivyotengenezwa kwa chuma na ngozi ya mbuzi. Wanaume pia hubeba viti vidogo (vinavyojulikana kama ekicholongs) na huvitumia kama viti kuliko kukeketi chini kwenye mchanga ulio moto wa mchana . Viti hivi pia hufanya kichwa cha mkaliaji kubaki kama kimeinuka kutoka mchangani na hivyo basi kuzuia mapambo yoyote ya kichwa ya kienyeji kuharibika. Pia, ni kawaida kwa wanaume kubeba rungu kadhaa; moja hutumiwa kwa kutembea na kusawazisha wakati wa kubeba mizigo, na nyingine, kwa kawaida nyembamba na refu, hutumika kuwachapia mifugo wakati wa shughuli ya ulindaji. Wanawake kitamaduni huvaa shanga, na kunyoa nywele zao kabisa ambayo mara nyingi ina shanga zilizofungiliwa mwishoni mwa nywele. Wanaume pia hunyoa nywele zao. Wanawake huvalia vipande viwili vya nguo. Kimoja kikiwa kimefungwa kiunoni huku kingine kikisitiri upande wa juu mwili.

Mifugo[hariri | hariri chanzo]

Waturkana hutegemea mito kadhaa, kama vile Mto Turkwel na Mto Kerio. Mito hizi zinapofurika, mchanga uliobebwa na maji ya mto pamoja na maji hujaza maeneo wazi mto na maeneo haya hulimwa baada ya mvua nzito , ambayo kutokea kwa nadra. Wakati mito inapokauka, visima wazi huchimbwa katika maeneo ya mito na maji yake hutumiwa kwa kunywesha mifugo na matumizi ya binadamu. Kuna chache,iwapo vipo, visima vizuri kwa ajili ya maji ya matumizi ya jamii na mifugo, na mara nyingi familia hulazimika kusafiri masaa kadhaa kutafuta maji kwa ajili ya mifugo yao na wenyewe.

Mifugo ni kipengele muhimu kwa utamaduni wa Waturkana . Mbuzi, ngamia, punda na ng'ombe wa zebu ndio kundi la msingi la mifugo wanaotumiwa na Waturkana. Katika jamii hii, mifugo sio tu kuwapa maziwa na nyama, bali pia kama aina ya sarafu inayotumika kwa ajili ya mazungumzo ya ulipaji wa mahari na kulipia mahari. Mara nyingi, kijana atapewa mbuzi moja wa kuanzia , na atalimbikiza zaidi kwa ufugaji. Kwa upande mwingine, baada ya kulimbikiza mifugo wa kutosha, mifugo hawa watatumika kulipia mahari kwa wake zao. Ni kawaida kwa wanaume wa Kiturkana kuwa na maisha ya bibi wengi, kwani idadi ya mifugo itaashiria idadi ya wake kila mmoja anaweza kulipia na kukimu.

Chakula[hariri | hariri chanzo]

Waturkana hutegemea mifugo wao kwa maziwa, nyama na damu. Waturkana mara kwa mara hufanya biashara na Wamasai kwa mahindi na mboga. Waturkana hununua chai kutoka miji na kuunda chai ya maziwa.Asubuhi watu hunywa uji wa mahindi na maziwa,na wakati wa chakula cha mchana na chakula cha jioni ,hula ugali wa mahindi kwa kitoweo. Zebu huliwa tu wakati wa siku kuu lakini mbuzi huliwa mara kwa mara. Nyama ya ngamia na samaki ni mwiko. Wanaume mara nyingi huenda uwindaji kushika swara, nguruwe wa mwitu,kulungu,sungura na wengine zaidi. Baada ya uwindaji, wanaume huenda tena kukusanya asali ambayo ndio kitu tamu Waturkana wanacho.

Nyumba[hariri | hariri chanzo]

Nyumba hujengwa kwa kutumia mbao na kisha kuvimbwa na nyasi na kisha kufungwa.Nyumba ni kubwa ya kutosha familia ya watu sita.Kawaida, wakati wa msimu wa mvua nyumba hufanywa kuwa refu na hufunikwa kwa samadi. Mifugo huweekwa kwenye zizi la mbao.

Hifadhi ya picha[hariri | hariri chanzo]

Angalia Pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Pavitt, Nigel (1997) Turkana. London: Harvill Press. ISBN 1-86046-176-X
  • Lamphear, John (1988) 'The people of the grey bull: the origin and expansion of the Turkana', in Journal of African History, 29, 1, 27–39.