Wagikuyu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Wagikuyu (pia: Wakikuyu) ni kabila kubwa nchini Kenya lenye watu milioni 7.5 au asilimia 22 za Wakenya wote. Hukaa hasa katika nyanda za juu za Kenya ya Kati katika mazingira ya Nairobi hadi mlima Kenya. Mlima huu katika lugha yao huitwa "Kirimanyaga" ambao mlima huu maarufu kwa kuwa na kimo cha juu ni mahali ambapo wazee, walitolea kafara mungu wao "Ngai".

Wenyewe hujiita Agikûyû; Kikuyu ni tahajia tangu zamani za ukoloni na kuandikwa pamoja na Gikuyu. Lugha yao huitwa Kikuyu ni lugha ya Kibantu.

Kihistoria, wagikuyu ni wakulima na inaaminika kwamba walitoka eneo la Kongo pamoja na makabila mengine ya kibantu. Baadhi ya makabila yenye lugha za karibu ni Wameru, Waembu na Waabagusii.

Tofauti na awali kwa miaka mingi wamejenga makazi kwingineko. Kama makabila mengi nchini, wao wanakabiliwa na tishio la kuacha tamaduni na mila zao. Wagikuyu wanaojulikana zaidi kimataifa ni

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]