Frederick Lugard

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Frederick Lugard

Frederick John Dealtry Lugard (22 Januari 185811 Aprili 1945), alikuwa mwanajeshi, mamluki, mpelelezi na mtawala wa koloni.

Alikuwa Gavana wa Hong Kong (1907-1912), Gavana wa mwisho wa Nchi Lindwa ya Nijeria Kusini (1912-1914), balozi wa kwanza (1900-1906) na gavana wa mwisho (1912-1914) wa Nchi Lindwa ya Nijeria Kaskazini na Gavana Mkuu wa kwanza wa Nijeria (1914-1919).

Alizaliwa Madras (Chennai), India, lakini alilelewa katika Worcester, Uingereza.[1]

Upelelezi katika Afrika Mashariki[hariri | hariri chanzo]

Lugard katika picha iliyochorwa na mwandishi wa jarida la Vanity Fair, mwaka 1895

Baada ya kuondoka Unyasa Aprili, mwaka 1889, Lugard alikubali kufanya kazi katika Kampuni ya Kifalme ya Kiingereza kwa Afrika ya Mashariki (IBEAC). Alifika katika mji wa Mombasa mnamo Disemba ya mwaka huo. Katika mwaka 1888, IBEAC ilikuwa imepatiwa idhini ya kifalme na Malkia Victoria ili kuangalia uwezo wa kupanua ushawishi katika Zanzibar na Uganda[2] na kulikuwa na nia ya kufungua njia ya biashara kati ya Ziwa Viktoria katika Uganda na bandari ya Mombasa. Kituo cha kwanza cha biashara kilikuwa Machakos. Walikuwa wakifika Machakos kupitia njia za zamani ambazo zilikuwa zikipitia Jangwa la Taru, lenye joto kali na vumbi jingi.

Kazi ya kwanza ya Lugard ilikuwa kutafuta njia ya kufikia Machakos ambayo haingepitia Jangwa la Taru.[3] 

Agosti, mwaka 1890, Lugard alisafiri kutoka Mombasa hadi Uganda. Alihakikisha utawala na ushawishi wa Uingereza katika Ufalme wa Buganda na kukomesha ghasia kati ya vikundi tofauti ndani ya ufalme.[4][5]

Alipatiwa jukumu la kufanya makubaliano na makabila ya wenyeji na kujenga ngome njiani ili kuhakikisha usalama wa ziara ambazo IBEAC ingefanya baadaye.[6] IBEAC ilifanya makubaliano kutumia hati rasmi zilizokuwa zimeandikwa na kutiwa saini na watawala na viongozi wa makabila, lakini Lugard alipendelea kufanya makubaliano ya undugu wa kuchanjiana, kwani aliamini undugu huo uliwasawazisha.[7] Aliingia katika makubaliano kadhaa kama hayo na viongozi wa makabila kati ya Mombasa na Uganda. Mojawapo ya makubaliano ya uchale ambayo ni maarufu yalifanyika mwaka 1890, katika Dagoretti, kati yake na Waiyaki wa Hinga.[8]

Lugard alikuwa mtawala wa jeshi katika Uganda kutoka Disemba 26, mwaka 1890 hadi Mei mwaka 1892. Wakati huo, alizuru Safu ya Ruwenzori hadi Ziwa Edward, akichora ramani ya maeneo hayo. Pia, alisafiri hadi Ziwa Albert akarudi na maelfu ya Wasudani ambao walikuwa wameachwa na Emin Pasha na Henry Morton Stanley wakati wa ziara yao.

Huduma katika koloni[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 1894, Lugard alitumwa na Kampuni ya Kifalme ya Nijeria aende Borgu, ambapo alifanya makubaliano na viongozi ambao walitambua utawala wa Uingereza. Kutoka mwaka 1896 hadi mwaka 1897, Lugard aliongoza msafara wa kuenda katika Ziwa Ngami, Botswana. Baadaye, alitumwa Koloni la Lagos na bara Nijeria ili aanzishe jeshi la wenyeji ili lilinde maslahi ya Uingereza dhidi ya Ufaransa

Baada ya kuhudumu katika Jeshi la Afrika Magharibi, Lugard aliteuliwa kuwa Balozi wa Nchi Lindwa ya Nijeria Kaskazini. Alisoma tangazo liliotangaza kuundwa kwa nchi lindwa katika Januari 1, 1900.[9] 

Lugard alifanywa shujaa wa ukoo bora mwaka 1901 kwa sababu ya huduma yake katika Nijeria.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Sir Frederick John Dealtry Lugard (1858-1945) - Find A Grave Memorial". 13 June 2018.  Check date values in: |date= (help)
  2. "The Imperial British East Africa Company - IBEAC", Softkenya.com, 2013-01-10. Retrieved on 2018-10-06. (en-US) Archived from the original on 2017-10-25. 
  3. Miller, Charles (2015). The Lunatic Express. London: Head of Zeus Ltd. 4022. ISBN 9781784972714. 
  4. The London Quarterly and Holborn Review (kwa Kiingereza). E.C. Barton. 1894. uk. 330. 
  5. Youé, Christopher P. (2006-01-01). Robert Thorne Coryndon: Proconsular Imperialism in Southern and Eastern Africa, 1897-1925 (kwa Kiingereza). Wilfrid Laurier Univ. Press. uk. 126. ISBN 9780889205482. 
  6. Nicholls, Christine Stephanie (2005). Red Strangers: The White Tribe of Kenya (kwa Kiingereza). Timewell Press. uk. 10. ISBN 9781857252064. 
  7. Charles., Miller, (2015). The Lunatic Express. Head of Zeus. uk. 4015. ISBN 9781784972714. OCLC 968732897. 
  8. Osborne, Myles; Kent, Susan Kingsley (2015-03-24). Africans and Britons in the Age of Empires, 1660-1980 (kwa Kiingereza). Routledge. uk. 1. ISBN 9781317514817. 
  9. "The Transfer of Nigeria to the Crown" The Times (London). Thursday, 8 February 1900. Issue 36060, p. 7.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Frederick Lugard kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.