Ziwa Viktoria

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Ziwa la Viktoria Nyanza
Ziwa Viktoria Nyanza jinsi inavyoonekana kutoka angani
Ziwa Viktoria Nyanza jinsi inavyoonekana kutoka angani
Mahali Afrika ya Mashariki
Nchi zinazopakana Tanzania, Kenya na Uganda
Eneo la maji 68,100 km²
Kina ya chini 81 m
Mito inayoingia Kagera, Katonga, Nzoia
Mito inayotoka Nile
Kimo cha uwiano wa maji juu ya UB 1,134 m
Miji mikubwa ufukoni Kampala, Kisumu, Mwanza
Ziwa Viktoria na Bonde la Ufa.
Ongezeko la msongamano wa watu kandokando ya Ziwa Victoria.
Lugha kandokando ya Ziwa Victoria.
Tofauti ya levo katika Ziwa Victoria.
Ongezeko la msongamano wa watu kandokando ya Ziwa Victoria likilinganishwa na lile la Afrika nzima.

Ziwa Viktoria (pia: Viktoria Nyanza, Ziwa Nyanza) ni ziwa kubwa la Afrika ya Mashariki lililopo baina ya Tanzania, Kenya na Uganda. Ni ziwa kubwa kuliko yote barani Afrika, na la pili duniani, baada ya Ziwa Superior ambalo lipo Amerika ya Kaskazini.

Ziwa Viktoria lipo mita 1134 juu ya usawa wa bahari na lina eneo la kilometa za mraba zaidi ya 68,100.

Maji ya ziwa Viktoria yanamiminika kwenye mto Nile na kuelekea bahari ya Mediteranea kwa umbali wa maili 4,000.

Ziwa hili linapata maji yake mengi kutokana na mvua (80%) na kutoka vijito vingi vidogo. Mto mkubwa unaoingia Viktoria ni Mto Kagera unaotiririka kutoka magharibi.

Ziwa Viktoria ni miongoni mwa maziwa yenye visiwa vingi vidogovidogo.

Ziwa hili lina kina cha wastani cha mita 40 na mwambao wa urefu wa kilomita 4,828, visiwa vyake vikiwa vimechangia 3.7% ya urefu huu.

Eneo la maji ya ziwa limegawanywa 6% (4,100 km2) nchini Kenya, 45% (31,000 km2) nchini Uganda, na 49% (33,700 km2) nchini Tanzania.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Africa satellite plane.jpg Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ziwa Viktoria kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.