Kisiwa cha Kome
Mandhari
Kisiwa cha Kome ni kati ya visiwa vya mkoa wa Mwanza, kaskazini mwa Tanzania.
Kinapatikana katika ziwa Nyanza, la pili duniani kwa ukubwa, maarufu zaidi kama Ziwa Viktoria.
Kisiwa kinakaliwa na watu toka makabila mbalimbali ya Tanzania; muingiliano huo unatokana na shughuli za uvuvi, hivyo maeneo kama Ntama, ambacho ndicho kitovu cha kisiwa, Mchangani, Nyalusenyi na Kabaganga yanaongoza kuwa na muingiliano mkubwa wa watu.
Wenyeji ni Wazinza. Japo Wasukuma na makabila mengine yapo kwa wingi pia.
Upatikanaji wa chakula ni wa kuridhisha haswa kwa kuwa wakazi ni wakulima na ardhi ni nzuri yenye rutuba na upande wa kitoweo wakazi ni wafugaji wadogowadogo na wavuvi, hivyo vitoweo ni vya kutosha.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mwanza bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kisiwa cha Kome kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno. |