Nenda kwa yaliyomo

Wazinza

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Wazinza ni kabila la watu kutoka eneo la kusini-magharibi kwa Ziwa Viktoria na visiwa vya jirani, nchini Tanzania. Lugha yao ni Kizinza.

Mwaka 1987 idadi ya Wazinza ilikadiriwa kuwa 138,000 [1]. Wazinza ni kabila dogo lakini lina mambo makubwa liliyoyafanya hapo kale; baadhi ya hayo ni uhunzi na ususi.

Kazi yao ilikuwa uvuvi, ufugaji na uwindaji pamoja na kilimo. Kwa sasa wamejikita katika anga la wasomi maana wametapakaa kila taaluma na kila mahali.

Vyakula asilia wanavyovipenda

[hariri | hariri chanzo]

Wazinza walio wengi hupenda kula ugali wa mhogo, ndizi, samaki (hasa sato, sangara, mumi, kamongo, dagaa, mbete, nshonzi) na nyama.

Lakini pia kutokana na uhaba wa vyakula hivyo na mgawanyo wa makazi na kazi, Wazinza wamekuwa wakila vyakula vya aina nyingine nyingi. Mfano ni wali, ugali wa mtama, ugali wa mahindi, mboga za majani kama vile msusa, kisamvu, mchicha, n.k.

Vyakula asilia kama maboga, viazi vitamu, mihogo mitamu, kunde, maharage ni miongoni mwa vyakula muhimu sana kwa Wazinza.

Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wazinza kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  1. [1]