Wawanda

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Wawanda ni kabila la watu kutoka kusini-magharibi mwa nchi ya Tanzania. Wanapatikana katika mkoa wa Songwe, wilaya ya Mbozi, hususani tarafa ya Kamsamba maarufu kama bondeni, yenye kata za Kamsamba, Chilulumo, Mkulwe, Mpapa na Ivuna.

Mwaka 1987 idadi ya Wawanda ilikadiriwa kuwa 24,000 [1].

Lugha yao ni Kiwanda, ambacho hakina tofauti na Kinyamwanga, isipokuwa katika matamshi tu; pia kinaingiliana sana na Kifipa. Kifupi Wawanda, Wanyamwanga na Wafipa ni watu wenye asili moja isipokuwa uongeaji wao unatofautiana kimatamshi lakini maana inabaki kuwa ileile moja.

Uwanda ni neno litokanalo na eneo husika, kwa maana ya watu wa tambarare ya bondeni.

Pia Wawanda hupenda kula samaki na nyama.

Wawanda mtoto akizaliwa, ndugu na majirani huenda kumsalimia mama mtoto wakiwa wamebeba pombe.

Flag of Tanzania.svg Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wawanda kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.