Pombe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Chupa za pombe kali aina ya Whisky.

Pombe ni kinywaji kikali chenye kilevi ambacho upitilizaji wa unywaji wake hupelekea hali ya kulewa na hatimaye tabia ya ulevi inayoleta madhara mengi kwa wahusika na kwa jamii.

Katika kemia, pombe ni mwambatanisho wa viungo asilia ambapo sehemu ya hydroxyl (-OH) group imeambatanishwa na kaboni.

Mfumo wa pombe katika kemia.

Historia ya pombe[hariri | hariri chanzo]

Kulingana na wanahistoria Donald Hill na Ahmad Y Al Hassan, utengenezaji wa pombe ulikuwa unajulikana na jamii ya Waislamu hata katika karne ya 18. Watu wa Persian Rhazes ndio wanakisiwa kama waliovumbua pombe aina ya ethanol.

Matumizi ya pombe[hariri | hariri chanzo]

Pombe hutumika sanasana kama kileo.

Pengine pombe humwagiliwa kwa mgonjwa ili kumfanya afe ganzi wakati wa upasuaji.

Hutumika pia kusafisha vidonda.

Madhara ya pombe[hariri | hariri chanzo]

Ulevi wa pombe husababisha maafa mengi, haswa unapokunywa kupindukia.

Huenda ukasababisha ajali na ndiyo maana sheria za nchi nyingi zakataza uendeshaji wa gari unapokuwa mlevi.

Unywaji wa pombe pia waweza kufanya mtu awe mzinifu bila hata kutumia kinga ili kupunguza hatari ya maambukizi ya maradhi mbalimbali.

Unywaji wa pombe umesababisha kusambaratika kwa familia nyingi maana watu hawasikilizani.

Pombe pia hufanya ini kuwa na kazi ngumu na huenda ikaleta ugonjwa wa cirrhosis.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Blank template.svg Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Pombe kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.