Wamachinga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Wamachinga ni kabila la watu wa Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Lindi, wilaya za Kilwa na Lindi.

Lugha yao ni Kimachinga.[1]

Inasadikiwa asili ya kabila hili ni kandokando ya ziwa Mkoe, hasa mto Mbwemkuru unapoingia baharini.[2]

Wamachinga katika biashara[hariri | hariri chanzo]

Wachuuzi aina ya Wamachinga huko Huaraz.

Kwa kipindi cha karne ya 20 na 21 wamekuwa maarufu katika miji mbalimbali kwa kuuza bidhaa, hasa nguo za mitumba, wakiwa wamezishika mikononi wakisaka wateja.

Hali hii imepelekea wafanyabiashara wa namna hiyo wote kuitwa Wamachinga ingawa baada ya muda mfupi mtindo huu wa biashara ulianza kuhusisha watu wa rika na makabila tofauti.[3]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Historia | Lindi Region". lindi.go.tz. Iliwekwa mnamo 2024-01-13. 
  2. "Wamachinga ni kabila la watu wa Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Lindi, wilaya za Kilwa na Lindi". JamiiForums (kwa en-US). 2021-10-25. Iliwekwa mnamo 2024-01-13. 
  3. Sauti Ya Ujamaa (2021-10-22). "Hoja Potofu Kumi na Tano Kuhusu Wamachinga". SAUTI YA UJAMAA (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-01-13. 
Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wamachinga kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.