Wangoni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Ngoma ya Wangoni nchini Tanzania

Wangoni ni kabila la watu wa Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Ruvuma, hasa upande wa Kusini wa Songea. Pia wako Msumbiji.

Lugha yao ni Kingoni.

Asili yao ni katika matembezi ya Wazulu walioenea kutoka Afrika Kusini wakati wa karne ya 19.

Wangoni wamelaumiwa sana kwa kujifichaficha kuonesha maarifa yao hasa katika sanaa ya muziki na maigizo. Ikumbukwe kuwa Wangoni waliowahi kuvuma katika muziki ambao wamekulia Songea kwao ni Bambo na marehemu kapteni Komba. Lakini katika utafiti uliofanywa na watu inaonekana kuwa Wangoni ni maarufu sana katika kuimba misibani; wana nyimbo nyingi za misiba na za sherehe. Pia katika sanaa ya muziki hupenda kujitokeza kama kundi: fuatilia ngoma zao kama Mganda na Kihoda.

Wangoni wamekuwa wakipotea na kupoteza uhalisia wao kwa sababu ya kulowea: wanakoenda kukaa hujichanganya mapema na tamaduni za makabila mbalimbali mahalia na kupoteza uhalisia wao. Kwa mfano leo kuna Wangoni Wamatengo, Wangoni Wanyasa, Wangoni Wampoto, n.k. Leo hii tunaweza kuwatambua Wangoni kwa majina yao tu ambayo mengi ni ya wanyama au viumbe hai kama Komba, Mbawala, Mapunda, Tembo, Nguruwe, Simba, n.k. Yote katika yote tuwakumbushe hawa watu wasione aibu kujitokeza na kuwa na mchango wao.

Flag of Tanzania.svg Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wangoni kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.