Wasuba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Wasuba ni kabila kutoka eneo la Ziwa Viktoria, nchini Tanzania, karibu na mpaka wa Kenya.

Mwaka 1987 idadi ya Wasuba wa Tanzania ilikadiriwa kuwa 30,000 [1]. Lakini wengi zaidi huishi nchini Kenya, idadi yao ni 129,000.

Lugha yao ni Kisuba japo wengi wao huongea Kijaluo, hivyo lugha yao iko kwenye hatari ya kutokomea kabisa. Wasuba wengi hujitambulisha kama Waluo kwani wameasili (wameathiriwa na kuridhia) mila na desturi za Kiluo.

Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wasuba kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.