Wakutu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Wakutu ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Morogoro, Wilaya ya Morogoro Vijijini, vijiji vya Ukutu, Ukutu Magogoni, Kidunda na vinginevyo.

Wakutu hawatofautiani sana na Waluguru na Wazaramo, na kama wao ukoo unafuata upande wa mama, yaani ukoo wa mama ndio unaoongoza familia na watoto wote wanahesabiwa kuwa wa ukoo huo.

Pia lugha yao, ambayo ni Kikutu, haina tofauti kubwa na Kiluguru na Kizaramo.

Mwaka 1987 walikadiriwa kuwa 45,000 [1].

Flag of Tanzania.svg Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wakutu kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.