Wahangaza

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Wahangaza ni kabila la watu wa Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Kagera, hasa kwenye wilaya za Ngara na Biharamulo. Nje na wilaya hizo wanaishi pia sehemu za Kigoma na Karagwe.

Lugha yao ni Kihangaza.

Kwa sehemu kubwa Wahangaza ni wafugaji na wakulima. Hapo mwanzo chakula chao kikuu kilikuwa ni ndizi kwa maharage, lakini hivi sasa wamejifunza kula vyakula vya makabila mengine pia kama vile ugali.

Wahangaza ni watu wenye utamaduni sawia na makabila mengi ya nchini Tanzania yenye kujumuisha mila na desturi zinazoelekeana. Haya yanadhihirika katika sherehe za ndoa, kuzaliwa watoto, vifo, matambiko, mavuno na hata kusimikwa kwa viongozi.

Sherehe hizo hufanyika kila tukio hili linapojitokeza na muktadha wa tukio husika likafanyika na kundi fulani kama vile ukoo na pengine kundi la watu fulani wanaofanya kazi fulani maalum kama tiba, ufinyanzi, kilimo ama ufugaji.

Flag of Tanzania.svg Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wahangaza kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.