Wilaya ya Biharamulo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Mahali pa Biharamulo (kijani) katika mkoa wa Kagera.

Wilaya ya Biharamulo ni wilaya mojawapo ya Mkoa wa Kagera, Tanzania kaskazini magharibi, yenye postikodi namba 35600 [1]. Katika sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 323,486 [2]

Wasubi, walio kundi linalohesabiwa kati ya Wanyambo, Wazinza, Wahaya na Walongo, ndio wakazi asilia wa wilaya ya Biharamulo,

Jina[hariri | hariri chanzo]

Inasemekana, asili ya jina Biharamulo ni neno la Kisubi "Niharemuno" likimaanisha "Ni mbali mno". Neno hilo lilikuwa jibu la mzee mmoja kwa Mzungu aliyemuuliza wakati wanasafiri pamoja kutoka Geita kwenda kijiji cha Nyarubungo kilichopo Biharamulo. Mzungu alimuuliza Mzee huyo, "How many kilometers from here to Nyarubungo?" yaani, "Kuna kilomita ngapi kutoka hapa kwenda Nyarubungo?" na mzee yule alijibu, "niharemuno" akimaanisha "ni mbali mno'.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Wilaya hii pamoja na Wilaya ya Karagwe zilianzishwa na kutangazwa rasmi na Gavana wa Kiingereza Richard Turnbull mwaka 1958.

Shughuli[hariri | hariri chanzo]

Uchumi ni pamoja na ufugaji wa ng'ombe na mbuzi, kilimo cha kahawa, migomba, mihogo, mahindi, maharage na zao la pamba katika maeneo machache. Shughuli nyingine za kiuchumi katika wilaya ya Biharamulo ni uvuvi, biashara na uchimbaji madini.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Flag of Tanzania.svg Kata za Wilaya ya Biharamulo - Mkoa wa Kagera - Tanzania Flag of Tanzania.svg

Biharamulo Mjini | Bisibo | Kabindi | Kalenge | Kaniha | Katahoka | Lusahunga | Nemba | Nyabusozi | Nyakahura | Nyamahanga | Nyamigogo | Nyantakara | Nyanza | Nyarubungo | Runazi | Ruziba

Flag-map of Tanzania.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kagera bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Wilaya ya Biharamulo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.